UWEZO_WAKO
Member
- Nov 17, 2010
- 39
- 4
Ni mfano mzuri sana kwa kweli. Siyo tu kujitolea kwake sehemu ya mshahara wake, bali tu kwamba ameanza kazi ya kushirikiana na wananchi kujadili na kutatua matatizo yao. Tumezoea wabunge wengi wakishachaguliwa wanatokomea.
Nitoe angalizo wakati tukifurahia hiki kitendo kizuri cha Mnyika kujitolea sehemu ya mshahara wake. Matatizo yako mengi sana katika jimbo lake. Utaratibu wa kujitolea mshahara unaweza kumkosanisha na wananchi ambao hatamudu kuchangia miradi ambayo ni kipaumbele zaidi kwao. Pia mshahara wake ukiisha kutikokana na kuchangia miradi, ataanza kukwepa mialiko ya wananchi. Ina maana kwamba moyo wake huu mzuri wa kujitolea unaweza kumkosanisha na wananchi, pengine kupelekea kutochaguliwa Tena 2015.
Sasa Kama hatachangia matatizo yatatatuliwaje? Aungane na Mdee kupitia mipango rasmi ya manispaa ya kinondoni kwa miaka iliyopita na ijayo (strategic plan). Wapitie mapato na matumizi. Bora wakose vikao vya bunge kuliko vya baraza la madiwani. Kisha wahakikishe kero zote za wananchi zinaingizwa kwenye mipango ya manispaa na kuhamasisha wananchi kusimamia utekelezaji. Hii Ina maana kwamba manispaa ya kinondoni Ina uwezo wa kutatua matatizo yote na mbunge akatumia mshahara wake kujikimu na kusimamia utekelezaji.
Mbunge siyo "strong room" ya jimbo! Tukimtaka kujitolea sana pesa, mafisadi watapitia hapo hapo. Tusijekuwa kama wale wazazi ambao humpenda mtoto asiye na shughuli yoyote rasmi lakini anawasaidia sana wazazi, pesa nyingi. Siku wakisikia mtoto wao kapigwa risasi kwenye tukio la wizi, hudai mtoto wao amelogwa!
Ni mfano mzuri sana kwa kweli. Siyo tu kujitolea kwake sehemu ya mshahara wake, bali tu kwamba ameanza kazi ya kushirikiana na wananchi kujadili na kutatua matatizo yao. Tumezoea wabunge wengi wakishachaguliwa wanatokomea.
Nitoe angalizo wakati tukifurahia hiki kitendo kizuri cha Mnyika kujitolea sehemu ya mshahara wake. Matatizo yako mengi sana katika jimbo lake. Utaratibu wa kujitolea mshahara unaweza kumkosanisha na wananchi ambao hatamudu kuchangia miradi ambayo ni kipaumbele zaidi kwao. Pia mshahara wake ukiisha kutikokana na kuchangia miradi, ataanza kukwepa mialiko ya wananchi. Ina maana kwamba moyo wake huu mzuri wa kujitolea unaweza kumkosanisha na wananchi, pengine kupelekea kutochaguliwa Tena 2015.
Sasa Kama hatachangia matatizo yatatatuliwaje? Aungane na Mdee kupitia mipango rasmi ya manispaa ya kinondoni kwa miaka iliyopita na ijayo (strategic plan). Wapitie mapato na matumizi. Bora wakose vikao vya bunge kuliko vya baraza la madiwani. Kisha wahakikishe kero zote za wananchi zinaingizwa kwenye mipango ya manispaa na kuhamasisha wananchi kusimamia utekelezaji. Hii Ina maana kwamba manispaa ya kinondoni Ina uwezo wa kutatua matatizo yote na mbunge akatumia mshahara wake kujikimu na kusimamia utekelezaji.
Mbunge siyo "strong room" ya jimbo! Tukimtaka kujitolea sana pesa, mafisadi watapitia hapo hapo. Tusijekuwa kama wale wazazi ambao humpenda mtoto asiye na shughuli yoyote rasmi lakini anawasaidia sana wazazi, pesa nyingi. Siku wakisikia mtoto wao kapigwa risasi kwenye tukio la wizi, hudai mtoto wao amelogwa! Kwani mnafikiri ilikuwaje Lowasa na Chenge wakapokelewa kishujaa majimboni mwao baada ya kutuhumiwa ufisadi?