Naibu Katibu Mkuu Chadema John Mnyika amezidi kuisambaratisha CCM kwa kuhutubia maelfu ya watu katika mkutano mkubwa wa hadhara unaondelea jioni hii hapa Busega.
Katika ziara hiyo Mnyika amefuatana na Katibu Mkuu BAVICHA Julius Mwita.
Mnyika ameendelea kulaani sera mbovu za CCM zilizosababisha umaskini mkubwa kwa wananchi.
Mnyika alilakiwa kwa kishindo kikubwa alivyoingia Busega kwa watu kadhaa kuchana bendera za CCM na kuzitupa barabarani huku wakiimba nyimbo za kuisifu Chadema na viongozi wake.
Amewataka wananchi kujiandaa kujiandikisha kwa wingi kwenye daftari la kudumu la mpiga kura BVR zikifika.
Ameionya serikali kutocheza na swala la uchaguzi mkuu
Nyamikoma hiyoooo
Hiyo hapo
Utaona kesho ACT nao wanapitia hapo
Asisahau NA kwakwe mwambie ubungo ajiandae kukaa bench...
Acha uongo, huo mnara wa simu nyamikoma uko maeneo gani?
Pole sana hatuna Malori yakubebea watu kama ccmZile fuso ndo hazipo tena hadi msimame kwenye stuli?
Nikiboko ya ccmMnyika ni shiiidaaaa!! HONGERA SANA MNYIKA tulimiss sana nafasi ya Naibu Katibu Mkuu!!
lile tawi linaloongozwa na mfalme --------- Zitto..
Msafara wa Naibu Katibu mkuu Chadema taifa Kamanda John Mnyika jana jioni walifanya mkutano mkubwa sana katika kata ya Nyamikoma jimbo la busega Mkoa wa simiyu.Mnyika akiongozana na viongozi mbali mbali akiwemo Katibu wa Bavicha taifa Mwita Julius pamoja na viongozi mbali mbali pia waliweza kufunguwa ofisi ya Bavicha jimbo la busega na kutoa elimu kwa viongozi wote wa Chadema kata na jimbo nzima ya Busega.