Mnyika awaondoa hofu wananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnyika awaondoa hofu wananchi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Jan 2, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,254
  Trophy Points: 280
  Mnyika awaondoa hofu wananchi


  na Andrew Chale


  [​IMG] MBUNGE wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), amewaondoa hofu wakazi wa jimbo hilo kufuatia matukio ya kihalifu yanayotokea mara kwa mara ikiwemo ya uporaji na mauaji.
  Mnyika aliyasema hayo alipozungumza na Tanzania Daima Jumapili, kufuatia vitendo vya kihalifu kushamiri katika jimbo hilo ikiwemo maeneo ya Kimara, Mbezi Temboni na Kibamba kwa wahalifu hao kuvamia na kupora mali.
  "Mpaka sasa mikakati tayari imeshafanyika, hivyo wananchi watulie kwa kipindi hiki kwa kuwa tunaendelea kuimarisha usalama wao na mali zao kwa kuhamasisha vikundi vya ulinzi vikisaidiana na Jeshi la Polisi" alisema Mnyika.
  Alisema kuwa Kamati Maalum inayoshirikiana na Jeshi la Polisi ilikaa na kuangalia uwezekano wa kuweka ngome maalum katika eneo la Kimara ambayo itakuwa na vikosi vya aina zote za jeshihilo pamoja na lile la shirikishi.
  Pia alitoa pole kwa familia ya mkazi mmoja aliyeuawa kwa kuvamiwa na majambazi nyumbani kwake ambapo mwanamke mmoja alipoteza maisha huku mume akijeruhiwa vibaya na kulazwa.
   
Loading...