Mnyika au Zitto kwa Urais

Avanti

JF-Expert Member
Aug 24, 2010
1,209
239
Mpaka juzi moyoni mwangu nilikuwa naamini Mnyika angefaa kuja kuwa Raisi wangu miaka ijayo. Hii ni kutokana na kuwa na wasiwasi kuhusu Zitto ambaye ni dhahiri, pamoja na umahiri wa kufanya kazi zake za siasa, nilianza kumshtukia kwa yeye kuonesha kupenda sana madaraka. Sasabasi hata Mnyika kwangu mimi naona ameonesha udhaifu mkubwa sana kuongea matusi ambayo hayakuwa na maana yeyote kuyasema kwani kwangu mimi naona yeye ndiye kawa dhaifu. Kwa nini nasema hivi? Nasema hivi kwa sababu nyingi tu ila leo hapa ninaeleze mbili tu ili niweze kuendelea na kazi zangu.

Ya kwanza, lugha aliyotumia haikuwa nzuri sana, yaani ile kumtaja kabisa jina "Raisi Kikwete ni dhaifu", mi nafikiri angetumia maneno haya "serikali na uongozi wake ni dhaifu" isingeniletea tatizo kwangu. Nasema hivi kwa sababu madhara ya matamshi yake kwa leo tunayaangalia vema tu kwa sababu ya upepo wa kisiasa kwenda vibaya kwa serikali ya chama cha JK. Naamini ipo siku, sio leo au kesho, mambo yanaweza kuja kugeuka, hapo ndipo tutagundua Mnyika hakuwa sahihi. Binafsi naamini matamshi hayo yanagusa mtu mwenyewe na sio chombo anachokiongoza ama kukitumikia na hivyo basi chuki iliyojengwa na maneno hayo inaingia moyoni na hata kama mtu hasemi amesononeshwa kiasi gani leo. Tena hapa namaanisha sie aliyesemwa tu amesononeshwa na maneno hayo bali hata wanawe, ndugu zake, marafiki zake na wafuasi wake wengi tu ambao wengine wapo CDM. Hilo limewakaa moyoni, bisha usibishe ndivyo ilivyo.

Sababu ya pili, bado naamini, kama mtu mmoja alivyokwishasema yawezekana Mnyika kalewa madaraka. Inawezekana kabisa ndivyo na ukizingatia hivi juzi kashinda kesi ya uchaguzi. Inawezekana kabisa muda huu ndiyo tutamwona Mnyika alivyo, kwani wakati amebananishwa na kesi michango yake ilikuwa mizuri sana na kila upande ulimwona yeye mzuri, yaani yupo rational. Hata Lukuvi alikiri juzi kuwa anamheshimi Mnyika. Sasabasi kwa kuwa kesi yake haipo tena, ingawa nasikia kuna rufaa, basi ameamua kujionyesha jinsi alivyo kwa sababu naamini angekuwa kishawahi tamka matamshi mabaya hivi huko nyuma nadhani angekuwa na wasiwasi Raisi huyo huyo ambaye amemwita ni dhaifu angeweza kuonesha asivyo dhaifu kwa kuingilia kesi yake na kumtoa katika ubunge. Sasa basi kwa sasa Raisi hana tena namna ya kudeal na Mnyika, inaonesha sasa Mnyika ataendelea kuonesha udhaifu wake, ambao kwangu mimi sasa naamini hanifai tena katika uongozi, na sitakuja kumpigia kura tena! I hate insults!
 
Lazima umchukie kwasababu amekua too honest! Kaongea ukweli unaouma kwa mtu unaempenda, lazima ikuume! What about wale waliomkinai JK, hawawezi kusema hayo unayoyasema wewe! Na kama sio dhaifu, adhihirishe tuone!
 
Hahaha.This is one of the poorest thread ever!nenda kwenye blog ya mnyika facebook uone tulivyompa tano kwa kuongea ukweli kwamba Rais kikwete''kama taasisi'' ni dhaifu.Na jamaa kuonyesha sio mnafiki akayarudia maneno yaleyale kipindi cha baragumu kinachorushwa na channel ten asubuhi.unafiki hauna nafasi duniani.Hata Yesu(simba wa Yuda) alipokasirika alitupa nje mali za watu wanaofanya biashara hekaluni...let call spade a spade!
 
Back
Top Bottom