Mnyika amshukia Ngeleja mikataba ya gesi, mafuta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnyika amshukia Ngeleja mikataba ya gesi, mafuta

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Serayamajimbo, Feb 23, 2012.

 1. S

  Serayamajimbo Senior Member

  #1
  Feb 23, 2012
  Joined: Apr 15, 2009
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika ametaka Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kuwajibika kwa kitendo chake cha kuendelea kuruhusu kusainiwa kwa mikataba katika sekta ya madini bila ya kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusishwa.

  Mnyika ambaye pia ni Waziri kivuli wa Wizara ya Nishati na Madini ametoa kauli hiyo jana, siku moja tu baada ya Waziri Ngeleja kutiliana saini kwa niaba ya Serikali na kampuni ya kuchimba mafuta na gesi ya Swala.
  Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, Mnyika alisema kasi ya uingiaji mikataba inayofanywa na Wizara hiyo bila ya kushirikisha Bunge ni hatari na kwamba hadhari inapaswa kuchukuliwa ili kuepusha uchumi wa nchi na haki za wananchi kuhujumiwa.

  "Tunapaswa kuchukua tahadhari juu ya kasi ya siku za karibuni ya Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini na taasisi zake kuingia mikataba ya muda mrefu ya utafutaji wa mafuta na gesi asili katika maeneo mbalimbali nchini, hii itaepusha uchumi wa nchi na haki za wananchi kuhujumiwa," alisema Mnyika na kuongeza;

  "Waziri Ngeleja anapaswa kuwajibika kwa kuendelea kuruhusu kusainiwa kwa mikataba bila Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusika katika hatua za awali za maandalizi ya mikataba husika," alisema.

  Mnyika alimtaka Waziri huyo mwenye dhamana katika wizara ya Nishati na madini kuueleza umma sababu za Serikali kuendeleza usiri wakati wa kuingia mikataba hiyo hata kwa wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi.
  Mnyika alionya kasi ya uingiaji mikataba bila uchambuzi yakinifu isipodhibitiwa kwa mwelekeo sahihi wa sera, sheria, mipango na usimamizi italeta athari kubwa katika usalama na uchumi wa nchi na maisha ya wananchi kwa ujumla.

  Mnyika aliitaka Serikali kusitisha shughuli za uingiaji mikataba mingine mikubwa ya madini, mafuta na gesi asili bila kuzihusisha Kamati za Kudumu za Bunge kwenye hatua za awali za maandalizi ya mikataba hiyo aliyodai ni mikubwa yenye maslahi mapana ya nchi na athari kwa wananchi wa maeneo mbalimbali.

  "Kwa utaratibu wa sasa kwa mujibu wa Sheria ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge ya mwaka 1988 pamoja na kanuni na taratibu za Bunge, kamati au mbunge anaweza kuomba kwa serikali kupitia kwa ofisi ya Bunge nakala ya mikataba baada ya kusainiwa," alisema Mnyika na kuongeza ,

  Lakini, Katiba na sheria hazikatazi Bunge kuisimamia Serikali kuanzia katika hatua za awali za maandalizi ya mikataba badala ya kusubiri kuisimamia Serikali katika kutekeleza mikataba mibovu iliyoingiwa bila ushiriki wa wananchi au wawakilishi wao ambapo aliitaka wizara kutumia fursa hiyo kulinda masirahi ya umma.

  Katika hatua nyingine, Mnyika alimshauri Rais Jakaya Kikwete kuiongoza serikali kufanya marekebisho ya sheria za utafutaji na uzalishaji wa mafuta za mwaka 1980 na pia kuharakisha kutunga sheria ya gesi asili ambayo hadi sasa haipo.

  Serikali imengia mktaba na kampuni ya Swala na kufanya mikataba ya utafutaji mafuta na gezi kwa hapa nchini hadi kufikia juzi kuwa 26.

  Chanzo:
  http://www.mwananchi.co.tz/habari/49-uchaguzi-mkuu/20442-mnyika-amshukia-ngeleja-mikataba-ya-gesi-mafuta

   
 2. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,800
  Trophy Points: 280
  Swala???? anzieni hapo.
   
 3. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #3
  Feb 23, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0

  Mnyika kaza buti, hata usipofanikiwa watz wanajua dhamira yako na ya Chadema kuwa tulipigania rasilimali za nchi yetu dhidi ya uporaji wa majambazi wawekezaji wanaoshirikiana na ccm. Vizazi vijavyo watasema kuwa akina Mnyika na CHADEMA walijitahidi wakashindwa, wataheshimu makaburi yetu.
   
 4. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  hivi huwa hamjiulizi kwanini rais hajamtimua Ngeleja mpaka sasa pamoja na maazimio ya bunge? hiyo ndo kazi aliyopewa na rais pamoja na mafisadi wengine kuhakikisha kuwa wanaingia mikataba ya kinyonyaji ya kutosha kabla hajaondolewa kwenye baraza la mawaziri.
   
 5. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #5
  Feb 23, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,788
  Trophy Points: 280
  Nina mashaka sana na hii sector na kwa kweli mashaka yangu yananisukuma niamini kuwa kuna watu wanagawana hizi concession za mafuta na gas kwa siri siri ndo maana wanasaini mikataba fastafasta. Na inawezekana kabisa wanaonufaika ni matapeli wale wale tuliowazoea
   
 6. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #6
  Feb 23, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Nchi inatafunwa mno kupitia mikataba mibovu! watanzania tuamke.
   
 7. nahavache

  nahavache JF-Expert Member

  #7
  Feb 23, 2012
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 869
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hii sector imejaa rushwa hii. Inatakiwa wale wote wenye uhusiano na Rostam kama Ngeleja (Mwanasheria wa Rostam) na wenye uhusiano na familia ya mkuu wa nchi waondoke ili haki itendeke
   
 8. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #8
  Feb 23, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Ngereja sijui lini atajifunza kila siku madudu haya ndio matokeo ya kupeana uwaziri kisa mnajuana jamaa boga
   
 9. ismathew

  ismathew JF-Expert Member

  #9
  Feb 23, 2012
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 254
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mikataba hiyo sio halali, ni kwa manufaa binfsi ya Ngeleja na Mramba, na sio ya kuwanufaisha Watanzania.
  Bali yanaongeza njaa kwa Watanzania, hiyo kampuni inayoitwa swala imetokea wapi, wakati
  mshauri wake Mramba, Hapo tayari mazingira yaliyokuwepo ni ya kuwaibia Watanzania.
   
 10. F

  FJM JF-Expert Member

  #10
  Feb 23, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Ngeleja anaweza ku-sign mkataba bila kupata baraka toka kwa boss wake?
   
Loading...