Mnyika aahidi kumchukulia hatua askari wa Bunge aliyemsukuma

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
Dodoma. Mbunge wa Kibamba (Chadema), John Mnyika amesema atachukua hatua kwa kitendo cha kusukumwa kilichofanywa na askari wa Bunge mwishoni mwa wiki.

pic+mnyikaa.jpg


Alisema atafanya hivyo mara baada ya kumaliza msiba wa mmoja wa waasisi wa chama hicho, Philemon Ndesamburo.

“Nitatoa tamko na kuchukua hatua nikimaliza msiba, leo (jana) na kesho (leo) nipo msibani huku Moshi, lakini nitafafanua na kuzungumzia hilo nikimaliza,” alisema.

Mnyika alitolewa bungeni kwa nguvu na askari wa Bunge baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kuwaamuru kumtoa ndani akidaiwa kukiuka kanuni za Bunge wakati akichangia mjadala wa Wizara ya Nishati na Madini.

Pia, mbunge huyo alipewa adhabu ya kutohudhuria vikao saba vya Bunge, huku askari hao wakimtoa ndani kwa nguvu na kumsukuma.

Ndesamburo, ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Moshi Mjini kwa miaka 15 mfululizo ataagwa leo katika Uwanja wa Majengo mjini Moshi na baadaye mwili wake utapelekwa nyumbani kwake ambako taratibu za mazishi zitafanyika kesho.

Wakati Mnyika akisubiri kumzika Ndesamburo, Chadema Wilaya ya Ubungo imelaani kitendo alichofanyiwa mbunge huyo ikisema hakikuwa cha kiungwana na kilikiuka hadhi yake.

Katibu Mwenezi wa Chadema wilayani humo, Perfect Mwasiwelwa alisema kitendo alichofanyiwa Mnyika kingeweza kumletea majeraha kama angeanguka kutokana na mazingira ya eneo aliposukumiwa.

Mwasiwelwa alisema mwanasiasa huyo anawawakilisha wananchi zaidi ya 78,000 hivyo Chadema inalaani kitendo hicho kwa sababu si cha utu.

“Alitolewa nje katika mazingira ambayo sio ya utu, sio ya Kitanzania, sisi kama chama ngazi ya wilaya tunasema hakikuwa kitendo cha kawaida kabisa,” alisema.

Wakati huo huo, wabunge wawili wa Chadema; Halima Mdee (Kawe) na Esther Bulaya (Bunda Mjini) leo watasomewa hukumu yao baada ya Kamati ya Kudumu ya Maadili ya Bunge kuwajadili na kumshauri Ndugai hatua sahihi za kuwachukulia.

Bulaya na Mdee watasomewa hukumu kutokana na kulivalia njuga suala la Mnyika kutolewa ndani ya ukumbi wa Bunge wakati spika alipoamuru atolewe na askari wa chombo hicho.


Chanzo: Mwananchi
 
Mnyika asipoteze muda kwa issue hiyo hakumbuki Sugu alivyobebwa msobemsobe.

Wale ni askari wanafanya kazi kwa weledi kama utaleta ubishi watatumia taaluma yao kutumiza goal yao.

Tii amri bila shiruti.
 
Mnyika asipoteze muda kwa issue hiyo hakumbuki Sugu alivyobebwa msobemsobe.

Wale ni askari wanafanya kazi kwa weledi kama utaleta ubishi watatumia taaluma yao kutumiza goal yao.

Tii amri bila shiruti.
 
Mwache apeleke ànakohisi atapata haki kwani akishindwa kuna hasara gani
 
Hata hivyo wabunge wetu wafanye mazoez kidogo,mwanaume inabid kujitetea kidogo,angerusha hata ngumi mbili tatu hv,kwenye pambano lolote si lazima kushinda,lakin uoneshe jitihada ya kujib mapigo,mnyika umewadhalilisha sana wanaume kwa jinsi ulivyokua mpole Ile siku,
 
Tunaongea sana hivi hakuna namna tunaweza kumalizana na watu type hiyo huku "nje" kitaani?
 
Jamani wale ni askari walopkea amri kwa boss wao hlf uchukuliwe km biharusi? Wamekula kiapo kutii amri hata kama wanakwenda kufa, hata hamuoni walivoambiwa nyinyi ni askari gani? Mi nadhani tujadili siasa ila askari watakuwa hawatendewi haki kulaumiwa.
Ndio kukusukuma??? Walishamtoa nje ssa kumsukuma ilitoka wapi??? Au order ya ndugai ilikuwa msukumeni akifika nje??? Lets get real jifunzeni kwa askari wa nje wanajua haki za makmatwaji sio nyie mnawasha watu mpaka makofi na mitama wakati hta mtu silaha hana
 
Mnyika asipoteze muda kwa issue hiyo hakumbuki Sugu alivyobebwa msobemsobe.

Wale ni askari wanafanya kazi kwa weledi kama utaleta ubishi watatumia taaluma yao kutumiza goal yao.

Tii amri bila shiruti.

Ukiwa madarakani huwezi kuona hiyo hali. Ila ngoja utoke madarakani ndio ujue mziki wa kudhalilisha wengine. Kamuulize Hosni Mubarak nk ndio utajua nasema nini.
 
Polisi wanajinajisi wanapoamua kuwa upande wa wanyonyaji na madhalimu badala ya kuwa upande wa wananchi wanaolipa kodi kuwalisha wao mpaka na hayo mabwana zao madhalimu. Ni huzuni.
 
Siro alisema huwa wanatumia mbinu yeyote ile ili kumtoa mtuhumiwa pale ambapo anatakiwa atoke. Angetii sheria bila shurti...yaani alivyoambiwa atoke yeye angeanza kutoka mapema km hapendi hekaheka. Tuwe watulivu, unaweza pigwa hata fimbo ukadharilishwa hata ukishtaki baada ya tukio...ile aibu ipo pale pale..watu wameiona. Pole sana Mnyika...
 
Jamani wale ni askari walopkea amri kwa boss wao hlf uchukuliwe km biharusi? Wamekula kiapo kutii amri hata kama wanakwenda kufa, hata hamuoni walivoambiwa nyinyi ni askari gani? Mi nadhani tujadili siasa ila askari watakuwa hawatendewi haki kulaumiwa.
Umemaliza yote hata nliyotaka kuongea mkuu sema kuna watu watakupinga ila uko right
 
Back
Top Bottom