CCM moshi mjini chukueni hatua dhidi ya kada wenu Ibraline

Oct 17, 2024
6
7
Jumanne wiki hii ndani ya ofisi za chama cha mapinduzi(ccm) moshi mjini,kulitokea tukio ambalo siyo la kistaarabu pale kada wa chama hicho,Ibrahim Shayo a.k.a Ibraline alipomporomoshea matusi makali mstahiki meya wa manispaa ya moshi,Zuberi Kidumo.

Tukio hilo lilitokea muda mfupi baada ya wawili hao kutoka ndani ya kikao kilichoitishwa na mwenyekiti wa chama hicho moshi mjini,Faraj Swai na kuhudhuliwa na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama akiwamo mkuu wa wilaya ya moshi.

Wajumbe wengine ni mbunge wa jimbo la Moshi mjini,Priscus Tarimo,mkuu wa usalama wa wilaya(DSO),mkuu wa polisi wa wilaya(OCD),katibu wa ccm wilaya pamoja na mstahiki meya mwenyewe.

tukio hilo limepokelewa kwa hisia tofauti na wanachama wa chama hicho ambao wamekitaka chama hicho kumwajibisha kada huyo kutokana na kitendo cha aibu alichokionyesha mbele ya umati wa watu wengi.

ikumbukwe kuwa kada huyo yupo chini ya adhabu baada ya kupewa onyo na chama hiho kutokana na mwenendo wake usioridhisha unaoenda kinyume na kanuni za uongozi na maadili za ccm na jumuiya zake toleo la mwaka 2022.

Baadhi ya wanaccm wanasema tukio hilo limekitia aibu chama cha mapinduzi chama kinachotajwa kuwa ni chama cha kwenye viongozi wenye kufuata maadili na miiko ya chama huku wakirejea tukio jingine la kada la chama hichio ambaye katika siku za hivi karibuni alimpiga meya huyo ndani ya ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya manispaa ya moshi.

Abuu Shayo,diwani wa kata ya Mji Mpya ndani ya manispaa ya moshi,alimshambulia meya huyo wakiwa ndani ya kikao cha baraza la madiwani wa manispaa ya moshi tukio linalotajwa kuwa la hovyo kuwahi kutokea .

Je baada ya kada huyo kuwa ndani ya adhabu ya kupewa onyo,ccm itachukua hatua gani zaidi ni suala la kusubiria na kuona
 
Tatizo la CCM Arusha na Moshi ni kuwa na mamluki wengi sana wa CHADEMA. Mnahujumiana sana. Ila kama ni Ibra Line mmiliki wa coaster za Arusha - Moshi naona ni mwendelezo wa wachaga kuabudu pesa ndo chanzo cha yote.
 
Uchaguzi uliopita 2020 ktk kura za maoni ndani ya chama hicho Ibraline ndo alikuwa wa kwanza lkn kamati kuu ikarudisha jina la pili Priscus Tarimo, sasa Jamaa nae anatetea ushindi wake this time around au aweke swahiba wake.....that's what is going on
 
Inawezekana pia labda alitumia rushwa kuhonga wajumbe. Kamati kuu ya CCM iko mbele sana ya muda na ina macho ya kuona kinachoendelea.
 
Tatizo la CCM Arusha na Moshi ni kuwa na mamluki wengi sana wa CHADEMA. Mnahujumiana sana. Ila kama ni Ibra Line mmiliki wa coaster za Arusha - Moshi naona ni mwendelezo wa wachaga kuabudu pesa ndo chanzo cha yote.
Ana coaster?
Unaropoka tu. Tumia ubongo
 
Back
Top Bottom