Kipilipili
JF-Expert Member
- May 25, 2010
- 2,272
- 1,882
Habari!
Kwa wale waliowahi kusoma UDSM (Mlimani) miaka ya nyuma huenda wanamkumbuka huyu kijana "sharobaro" muuza karatasi ambaye inadaiwa ni "mnyalu" kutoka kule Iringa.
Alichokuwa anafanya ni kununua rimu kisha anabana karatasi 4 au 5 na kisha anauza kwa sh 100 (kwa wakati huo, sijui sasa kama bado anauza).
Wengi walimchukulia kama "muhuni" flani mganga njaa lakini mimi namtazama kama mjasiriamali alieiona fursa na kuitumia tena katika jumuia ya wasomi ambao wengi wao hawakuiona kama ni fursa au kama waliiona basi waliidharau na kuona kuwa wao ni wasomi hawawezi kufanya biashara "kichaa" kama ile.
Tumfanyie makadirio madogo;
Bei ya Rimu 1 aina ya MONDI = 6000
Rimu ina karatasi 500
Yeye anabana karatasi 4
Hivyo 500÷4=125 bundles
1 bundle=100Tsh
125 bundlesX100=12500 Tsh (mauzo)
Faida; 12500-6000=6500TSH(faida ya rimu moja tu)
Je akiuza rimu mbili kila siku kwa mwezi atakuwa na faida ya sh ngapi?
6500tsh X2 X5(working days) X4 Weeks=260,000Tsh
Tunajifunza nini kutoka kwa bwana "mnyalu"?? Mnyalu hana degree kama walivyo wengi wa wateja wake, wengine wana masters na hata Phd lakini mnyalu ameona fursa ndogo na kuitumia.
Je ni graduates wangapi wako mtaani wanashinda kuangalia TV kwa kisingizio cha kukosa ajira na hawaingizi hata alfu 10 kwa mwezi? jibu ni rahisi: HAWAWEZI KUFANYA KAZI HIYO kwa sababu si status yao, wao wana degree!!
Graduates wakiacha superiority complex waliyonayo basi nina hakika Macho yao YATAFUNGUKA na kuona Fursa nyingi zinazowazunguka ambazo nyingine hazihitaji mtaji mkubwa. Huu ni mfano tu mdogo kutoka kwa bwana "mnyalu", vipo vingi ambavyo graduates wanaweza kuvifanya individually au in groups
Ukiwa gradute unaweza kuiboresha wazo la biashara anayoifanya "mnyalu" na kulifanya kuwa ni wazo bora likakuingizia kipato zaidi.
Mfano:
1. Chukua begi lako la mgongoni ulilokuwa unatumia chuo
2. Chukua kiwi na brash unayoitumia kung'arisha viatu vyako
3. Nunua rimu mbili
4. Nunua staple machine ndogo
5. Nunua box la kalamu ya blue na nyeusi
6. Nunua karanga kg1, kaanga na funga kwenye vipakiti
7. Nunua BIG G/PK
8. Nenda ofisi za Tigo na ungainishe line yako na huduma ya kuuza Tigo Rusha (kuunganishwa ni bure)....uza Tigo Rusha
Weka vitu vyote kwenye begi na zunguka maeneo ya chuo na anza kutoa huduma.
Mtaji ukikua nunua mashine ya KUPIMA UZITO, weka kwenye bag na anza kutoa huduma....believe me wadada wanapenda sana kupima uzito ili kudhibiti miili yao isinenepe hovyo.
Kwa kifupi utakuwa unauza vocha, kung'arisha viatu vya wanafunzi, kuuza bites, kuuza kalamu na karatasi, kupima uzito n.k.
Je kwa mwezi utakuwa unaingiza kiasi gani??
Jitahidi kujenga uhusiano mzuri na wateja wako, ikiwezekana tengeneza business card ioneshe kiwango chako cha elimu, believe me utapata connection humo humo kutoka kwa wateja wako mana wengine wana makampuni yao na watavutika tu na uthubutu wako na wangependa ufanye nao kazi.
Biashara hii mtaji wake ni MDOGO SANA. Ondoa aibu, Superiority complex na acha kukaa nyumbani bila kazi..