Mnayasababisha wenyewe... acheni chokochoko

happiness win

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
2,461
1,384
Wenzangu, watu wengi huyajua mapungufu ya wanaume/wanawake wanaotaka kuwaoa/kuolewa nao na hukubali kuolewa/kuoa kwa kujifariji watayavumilia ili mradi tu waingie kwanye ndoa.

Baada ya muda chokochoko zinaanza... oooh ana kibamia.... ana kikwapa..... mlevi..... ana bwawa... mbinafsi....lo lo lo lo. Jamani kama uliamua kuyavumilia endeleaa hadi kifo kikutoe huko (kwa wale walioapa hivyo) kuanza kulalamika hakukusaidiii zaidi ya kuendelea kukuongezea machungu maana unayachochea.

Tahadhali kwa ambao bado hawajaingia kwenye ndoa.

Usijifariji na kujifanya mvumilivu kwa kero unayoiona kwa mwenza wako.... ukigundua kero ambayo haiwezi kurekebishika na itakukosesha raha maisha yako yote ikwepe mapemaaaa usijifanye mshindi na usiangalie sifa ya kuonekana umeoa/umeolewa leo angalia utaishije kesho.

Kumekuwa na na malalamiko mengi siku hizi kwa kuwa watu wanalichukulia jambo la kuoa?kuolewa kirahisi rahisi tuuuuuu.

Najua yapo matatizo ambayo huwezi kuyaona kwa macho na yanaweza kutokea ndani ya ndoa... kwa hayo huna ujanja utatafuta mbinu ya kuyatatua.

Huo ni mtazamo wangu... wewe unasemaje?
 
^^
Hata mimi, nafikiri sawa na wewe! Wachumba wakijipa muda wa kutosha..dalili za makucha huonekana.
^^

Sawa kabisa. Na tunapaswa ukiona yale makucha, mapenzi yasikutie upofu ukayapotezea baadae utajuta
 
Kumekuchaa!

Watu wengi tunaoana kistrategic! Upendo upo wa kubeep beep! Ukimpata fogo au average Joe, shughuli anajitahidi tahidi kupiga mzigo kama mheshimiwa machemlikibatari, ana kafurure basi UNAJIRIDHIKIA! Maisha yenyewe yako wapi ya ku DREAM BIG!? Unajitoa mhanga potelea pote!

Ila kiukweli if yuo have the LUXURY and just a little help from the heavens, inatakiwa umpate TRUE LOVE wako ambae ni myth! Wengi tunasurvive tu ila kuna wenye bahati wachache wanaishi na they have the LUXURY TO TASTE TRUE LOVE!

Ambapo mtu unapendwa DESPITE ANYTHING AND EVERY THING! Blindly in love wanasema! Haya mambo ya kumuona mwenzio kibamia, sijui ulimkubali kimakosa, ana kubwa kuitumia hawezi, mbaya, amekulostisha kimaisha ulitakiwa ufike mbali zaidi ya hapo asingekioa NI FRUSTRATION TU ZA MAISHA! Yule yule kibamia akishinda uraisi unaanza kuhisi genye juu yake! Unajiponheza kwa choice nzuri!
 
Well said dada.... people use to blink in their life..... but ma advice never blink in any decision you make in your life no matter what....
 
Mimi kama hunifai au sikufai nitakuambia mapema. Ila anaefaaa nitaendelea nae
 
kwa utaratibu huo, sijui kama ntaoa maana huyo mkamilifu pa kumchongea sina
 
Mimi kama hunifai au sikufai nitakuambia mapema. Ila anaefaaa nitaendelea nae

Kuna wakati unampata mtu ambaye yuko sawa sawa na mahitaji yako kwa tabia na kipato na mengine ila pengine kitu kimoja tu... let say kibamia (nimetolea mfano huu maana naona wengi wanalalamika) wakati unajua kabisa hakikutoshi sasa kwa nini ujiingize maana hii itakuwa mwiba wako milele. lazima ufanye uamuzi na ukiamua usilalamike.
 
Tatizo linaanza pale unapoanza kuwa na mahusiano na watu wengi, hapo ndio unajau kuhusu kibamia na zilizo kubwa. Ukijitunza hadi kuja kuolewa hayo yote hutakuja yapata. Tatizo kubwa ni kujaribu kama spana.
Mimi mtu kama yuko sawa leo kesho asipokuwa sawa ni wajibu wangu kumsababisha awe sawa kwa kujua tatizo na baadae suluhisho la hilo tatizo
 
kwa utaratibu huo, sijui kama ntaoa maana huyo mkamilifu pa kumchongea sina

Rafiki Mapi nani kasema kuna aliyekamilika??? hakuna hata mmoja ila kuna ambaye tabia zake na maumbile yake utaweza kuyavumilia na mtaishi kwa raha mkirekebishana dosari ndogo ndogo na kuchukuliana bila kelele wala matangazo. Hapa naongelea lile ambalo unaliona kabisa hutaweza kulivumilia. Tena wakati wako wa kuoa umekaribia nasubiri mwaliko....
 
Last edited by a moderator:

Hilo nalo neno.... Ukionja mboga nyingi utachanganyikiwa mazima
 
kwa utaratibu huo, sijui kama ntaoa maana huyo mkamilifu pa kumchongea sina

^^
Hatusemi upate mkamilifu,,tunamaanisha ujipime kama udhaifu wake unaweza kuubeba. Ukiona huwezi, off you go! Wahenga walisema, Ukitaka kuruka agana na nyonga.
Btw:
Mapi habari ya miezi mingi?
^^
 
Last edited by a moderator:
Rafiki Mapi nani kasema kuna aliyekamilika??? hakuna hata mmoja ila kuna ambaye tabia zake na maumbile yake utaweza kuyavumilia na mtaishi kwa raha mkirekebishana dosari ndogo ndogo na kuchukuliana bila kelele wala matangazo. Hapa naongelea lile ambalo unaliona kabisa hutaweza kulivumilia. Tena wakati wako wa kuoa umekaribia nasubiri mwaliko....

linalovumilika leo kesho linaweza nishinda, na nilie muacha leo kwa kushindwa kumvumilia kesho nitamtamani baada ya kukosa wa kumvumilia
kuhusu kuoa ngoja nifikirie kama nimefikia, ntakualika usijali
 
^^
Hatusemi upate mkamilifu,,tunamaanisha ujipime kama udhaifu wake unaweza kuubeba. Ukiona huwezi, off you go! Wahenga walisema, Ukitaka kuruka agana na nyonga.
Btw:
Mapi habari ya miezi mingi?
^^

Mungu ananipigania kaka. kwema?
ntajaribu kaorodhesha ninayoweza kuyavumilia maana kosa likitendwa na "A" leo kesho akitenda "B" hukumu yangu inakuwa tofauti, sijui kwanini. au ndio mahaba niue?
 
Kwa kweli kama kuna vitu unaona utaweza kuvivumilia adi kifo iwe tabia , au maumbile endelea.Kama tabia au maumbile ya mtu huwezi kuvumilia basi tafuta kwingine.Tatizo watu wana haraka sana.Jamani hamna mkombozi wa mchumba espesially katika tabia.
 
Back
Top Bottom