Mnawezaje kurudiana na 'EX' zenu?

Mnawezaje kurudiana na 'EX' zenu?

Katika kitu kimenishindaga kwenye mahusiano ni kurudiana na ex wangu yeyote yule. Mimi roho yangu ni ndogo sana mtu akinikosea huwa inaniwia vigumu kumsamehe na kurudiana nae.

Niliwahi kujaribu lakini tulikutana tu mara moja nikagundua sina hisia nae tena wala mapenzi hakuna.
Tangu lini matapishi yakalambwa? Ama kinyesi kikarudishwa tumboni?
 
Inategemea mliachanaje mkuu!

kuna ile mnaachana kama hamjaachana vile.. hii rahisi sana hata kupiga mechi za kirafiki..

Kuna ile mnaachana standard hii ina nafasi ya kurudiani ( kuna mahala mnashindwa kukubaliana, mnaamua kila mtu apite kushoto )

Kuna ile mnaachana kwasababu ya watu

kuna kuachana kwa vita hii nadra sana kurudiana japo hutokea

kuna kuachana kwa kuuana, na kuwindana hii haiwezekani kurudiana maana ukifanya kistake unaliwa kichwa..

EX huwa anakuwa mtamu kinoma, hasa kwenye part ya maongezi wakati unamkomesha
Kwenye utamu wa X, hilo halina pingamizi!

Na hiyo ndiyo huwa sababu kuu ya kurudiana na zingine ni uzushi tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom