wawe wanaangalia namna ya kulinda brand yao kwa mistake zao,kuliko kuwakarahisha wateja mpaka kupelekea kumfukuza mtu kurudi kwenye mitandao mingine...pia wajue vifurushi vyao havina tofauti na tigo wala voda kwa gharama
Hivyo wasijidangaye kwamba itakuwa ngumu watu kuwakimbia..maana kwa na namna yoyote hawawezi kuifika voda wala tigo ikiwa kila kitu wanafananao..tena wenzao wanajitahid Bando za internet hazikati kiboya boya kama wao
Mkuu hii kitu hii tulishaiangalia kwa tathimini siku nyingi sana tukaamua kunyamaza tu!
Unakumbuka kabla ya Magufuli kuivunja menejimenti pamoja na 'director', huko nyuma kulikuwa na simu pamoja na line za mtandao mmoja, unajua madhumuni yake yalikuwa ni nini!
Hiyo ilikuwa ni hujuma ya kifisadi kuihujumu Ttcl kibiashara, holo kila mtu anajua na Magufuli alishawahi kuliweka wazi siku1.
Sasa yalipokuja mabadiliko ya menejimenti na huyo mkurugenzi Kindamba na slogani yao ya' rudi nyumbani...' tukajua kuwa mabadiliko chanya yaja, lakini wapi!
Kumbe ile kampeni ya hujuma ya kuiua Ttcl bado inaendelezwa hadi sasa, lakini imeboreshwa kisayansi kwa kutoa gawio na kuikunja makucha serikali.
Ukiuliza faida ya kutoa hadi gawio wanaitoa wapi, wanajibu kiurahisi tu kwamba wanaipata kwa kuuza masafa kwa makampuni mengine ya simu!
Huku kubweteka kwao usidhani hawajui ama hawawezi kubuni ushindani wa kibiashara, wanajua sana na ni makusudi kama ilivyokuwa kwa shirika ka reli, liliachwa life ili wenye magari wafanye biashara.
Haiwezekani kama shirika kubwa kama hili la umma likashindwa mikakati ya kuboresha huduma za mawasiliano ya simu likabaki na sura ya kizamani kama lilivyo Ttcl sasa, lazima kuna kitu nyuma ya pazia.
Ttcl imebakia ni ya wazee, ukienda maofisini unakutana na vimbabu/vimbibi ama viti vilivyoachwa wazi na staff waliostaafu kwa umri bila ya kujaza nafasi kwa kuajiri vijana wapya!
Kutoa gawio kwa serikali imekuwa ndiyo kinga kuu ya kuhujumu watakavyo kwa kuwa hakuna wa kuwauliza.
Lakini nasema kila siku kwamba ipo siku yao, tuliona mambo kama hayo kwa Mchechu wa Nhc, nini kilimtokea na leo yuko wapi.
Sent using
Jamii Forums mobile app