Mwene chungu
JF-Expert Member
- Nov 12, 2016
- 915
- 752
Habari !!
nakumbuka wakati
Mawazo ameuawa na kukatokea shida kidogo wakati wa kuuchkua mwili wake ili ukazikwe kila mtu alisema lake.
Yamepita mambo kadhaa hapa katikati,sema mengine huwa hayavumi(hayasikiki)kwa sababu wanayoyapata hayo si watu maarufu.
Mara ikaja issue ya Ben Sanane akapotea wapo waliosema mengi kuwa amejipoteza mwenyewe.Na hadi sasa haijulikani aliko.
Juzijuzi huko Mkuranga wameuwa wenyeviti wa serkali za mitaa kadhaa na maafisa misitu hadi sasa hatujui nani anatekeleza haya.
Jana Roma na wenzake amepotea hatujui hadi sasa kama wako hai,mahali walipo vyote ni kitendawili.Binfsi siamini kama Roma hatapatikana.
Cha ajabu sana wapo watu wanafurahishwa sana na hali hizi,kauli zao na maandishi yao yanalionesha hili hasa huko mitandaoni
.Mim sjui wanafaidika vipi na kupotea kwa hawa Watanzania wenzetu.