Mnaomiliki gari za kimarekani zina changamoto gani?

Mmmm V 8 na V 10 engine huku shidaaa sio size yetu.....Escalade na GMC ?
 
Gari zote za kisasa hata za kimarekani makampuni yote yanajitahidi kutengeneza yasiyo kula mafuta mengi ili kumiliki soko fuel economy cars.

Kwa sasa ukitengeneza magari yanayokunywa mafuta mengi fuel guzzling cars ndio hivyo tena huwezi kushindana kwenye soko kwa sababu bei za mafuta zimekuwa juu mno. Kuna aina ya magari zaidi ya kumi yanayotengenezwa nchini Marekani.
 
Shida kubwa tatu ya kwanza upatikanaji wa spea mgumu,ya pili upatikanaji wa mafundi .Waweza Pata miji mikuu nao wachache sana na Huwa hawataki Vizuri ukisafiri nalo mikoani likikuharibikia utaliweka kwenye mawe.Tatu yanaharibika upesi sababu ya barabara zetu mbovu.Hayajatengenezwa kuhimili changamoto ya barabara zetu kama za kwetu Afrika
Nne ulaji wa Mafuta yanakula Mafuta kama majini

sita mengi makubwa na marefu kwenye maeneo ya mijini yenye parking ndogo ndogo kuyapaki changamoto na uendeshaji wake barabara za vichochoroni laweza shindwa kuingia au kukata kona
 
kwaiyo nijichanganye nione kitatokea nini?

Si lazima iwe changamoto...

Fikiria tu katika kuendesha, then ukagongwa kitu kidogo tu kama front or rear bumper kiasi kwamba haliwezi tengenezeka tena, unahisi utalipata wapi bumper jipya au hata used kama sio kuanza kuagiza nje na kupark gari maskani?
 
Wakuu kuuliza sio ujinga.
Ni mazuri mkuu azima siku hata Jeep Grand Cherokee moja la mtu uendeshe upate Hemi la 5.7L, 6.2L au 6.4L

Kuhusu mafuta usituulize.

Ukiweza kujichanga Nunua Wrangler miaka michache nyuma ilikuwa ndio gari yenye depreciation value ndogo kuliko gari yoyote hata Toyota zilikuwa hazitii mguu.

Sijui kwa sasa.
 
Japo sina gari ila uzoefu wangu high end cars zinataka atleast usiwe na hela za mawazo.
Maskini wengi wapo kwenye toyota.
 
Back
Top Bottom