Mnaombeza JPM mkumbuke mlikotoka.

Mnaombeza JPM mkumbuke mlikotoka.

Hivi punde nilikuwa nasoma maoni ya watu kuhusu JPM kuwa hajui kuzungumza Kiingereza/Kiswahili fasaha.

Ningependa kuwakumbusha Watanzania wenzangu kwamba kwa sasa kuna mambo muhimu zaidi ya kufuatilia kuliko mjadala huu wa lugha. Pia naomba mkumbuke kuwa kabla ya utawala huu tumeshapoteza miaka 10 bila ya kuwa na rais. Kwahiyo, tutumie changamoto ya awamu hii ya 5 kushirikiana kulijenga taifa.
Watu ndio sisi sisi. Tukimpata rais msukuma sawa, tukimpata mmasai sawa. Tukimpata msambaa kama januari hata kiswahili anaongea kama mzungu ndio tutasema sawa?
 
wengine nao waambiwe tu wamepost..
Nyerere ndie aliekua na uzalendo kwa wananchi..
mwengine anajisikia tu uishi maisha magumu ndio raha yake..
ndio maana wengine wake zao wamejaa ngeu na kutabasamu walishasahau..
eti napenda waishi kama shetani..
duh
 
Kuna Mwandishi mmoja wa nje (jina na chombo nimesahahu), miaka ya mwishoni mwa 90 alitusifu watanzania kwa utulivu na amani baada ya kudai kuwa eti nchi ilikaa bila Rais kwa miaka 10 lakini ikabaki salama. Alishukiwa kama mwewe
..........ndo historia yetu?
 
Mkuu punguza ushabiki uliopitiliza..,
Plse litendee haki Jukwaa letu hapa JFs kw kujitahidi kujituma ktk kufikiri...

Nchi yetu toka tupate uhuru zaidi ya miaka 50, tumeongozwa na 4 Presidents, na mwaka jana amepatikana wa 5.

Watanzania wanastahili kuishi maisha yenye ustawi mzuri na kutumia haki zao za msingi, pamoja na kutoa maoni yao khs Viongozi wa Nchi hii.
Tatizo liko wapi, yeye anaona hivyo
 
Kuna mtu amediriki kumlinganusha JPM mwenye PhD na Mbowe anayesemekana kupata Division Zero Form six.
 
sishangai unaishi kigamboni na soon unapita kwenye daraja ulilolijenga huyo unayemtukana. ukiumwa moyo unakimbizwa kwenye taasisi ya moyo aliyoipigania huyo unayemtukana, ukitaka kwenda kuona ndugu zako kanda ya ziwa hupiti nchi jirani kwa juhudi za huyo unayemtukana. Haishangazi umesoma shule za kata alizozijanga huyo unayemtukana na ukagraduate pale UDOM ambazo ni juhudi za huyo unayemtukana kitu ambacho hakikuwepo hata kwenye ilani ya chama alichopewa dhamana kukiwakilisha. bila shaka utakuwa bwabwa wewe.
Juzi JK alisema kuwa ana raha kupumzika. alisema kuwa maisha yake ya sasa ni ya raha tu kwani hasomi tena mafaili.
Alisema huwa anafanya kazi nyingi za kimataifa.
Kusema hivi ni kumaainisha kuwa kazi ya urais ni kubwa.
Mimi naona kuwa kuna mengi allifanya na kupigiwa mfano kuna pia aliyotetereka lakini kusema hatukuwa rais ni joke kwa kweli. Tumwache apumzike
 
Elimu bado ni tatizo,vitu vingine ambavyo vinatakiwa vifanywe na serikali unaona kama neema.Huu ni ulimbukeni,uozo ulioonekana kwa kipindi kifupi ni mkubwa sana.Hata mnyika aliwahi kusema tumefika hapa kwasababu ya udhaifu wa JK.Mtu amekopa akajenga hayo madaraja,hiyo hospitali na hicho chuo ulichotaja,bado deni ametuachia sisi wananchi,hapo unasifia nini?Kukopa?Nani atashindwa kukopa na kujenga?Nchi hii ilimshinda kukusanya kodi hasa alipoweka uswahiba mbele kwa kuteua kijamaa,matokeo yake nchi ikazidi kudidimia huku deni likipanda.Huyu hajafanya jambo la kustahili kupongezwa,hata bila Rais,tungekuwa na waziri mkuu tu basi tungekuwa mbali zaidi ya hapi.Watu wanaiba pesa wanasamehewa,kila mtu anajichotea kadri awezavyo,ufisadi kila kona,huyu alikuwa rais au msanii?He is the worst president ever in the history of Tanzania,period
nimesema sishangai na wewe ni graduate wa UDOM aliyoijenga huyo unayemtukana. sisi tuliozaliwa zamani kidogo na tuliosoma hapo kabla tunajua ilivyokuwa ngumu karibia kwa kila kitu. mfano, kwenda sekondari ilikuwa ni kitu cha kufikirika na pengine hakiwezekani kwa baadhi ya jamii. kusafiri ilikuwa ni shida ndani ya nchi maana kuna kipindi ilibidi upange siku 2 kufika huko uendako ndani ya jamhuri hii. usifikiri tunamsifia Kikwete bure, tunaona na kufaidi aliyoyafanya. (yeye kama binadamu hakosi mapungufu mfano ni hilo la ukusanyaji wa kodi, lakini huyo jamaa kafanya vizuri sana kuliko watangulizi wake wote 3). miaka michache sana baadaye njoo usome ulichoandika. maana hapo ndo uelewa wako ulipoishia.
 
Mimi si mwanaCCM na ninaichukia sana CCM kama adui namba 1 aliyeififisha safari ya maendeleo ya Watanzania. Lakini kuna mambo naweza kumpongeza Kikwete.

Kikwete alikuwa dhaifu sana katika uteuzi maana hakuwa na vigezo sahihi, badala ya kimteua mtu kwa merit, kigezo chake kikuu ilikuwa uswahiba na undugu, na hilo lilimharibia sana. Aliwajaza marafiki na ndugu kwenye serikali yake wasiokuwa na uwezo wowote.

Magufuli alistahili.kuacha mambo yote ya kipumbavu ya utawala wa Kikwete lakini alistahili kuendeleza mambo mazuri ya utawala wa Kikwete, hasa kwenye mahusiano ya kimataifa.

Utawala wa Magufuli unaonekana kufanya vizuri kwenye nidhamu, kuzuia ubadhirifu, matumizi mazuri ya rasilimali za Taifa, kupiga vita rushwa na uwajibikaji lakini imeonesha kuboronga sana kwenye demokrasia, utawala wa sheria, ujenzi wa mifumo ya kiutawala na kulinda haki na uhuru wa Raia. Utawala wa Magufuli ulikuwa na nafasi kubwa zaidi ya kufanikiwa kuliko utawala wa Kikwete lakini akiwasikiliza waimba mashairi kama akina Polepole kuwa Tanzania haihitaji mahusiano mazuri na jamii ya kimataifa, anaweza kuboronga kuliko Kikwete.

Mataifa ya Magharibi yana uwezo wa kufaidiki rasilimali za.Afrika bila ya kulazimika kutoa misaada. Watu wenye uelewa mdogo hawawezi kulielewa hilo.
angalau wewe umeandika kitu kinachoeleweka kidogo. tatizo la Kikwete lilikuwa kwenye kusimamia ukusanyaji wa kodi na kuweka nidhamu kwenye utumishi basi. mengine kafanya vizuri sana. mfano miundombinu ya barabara, mashule, mavyuo, mahosipitali, maji, umeme, utawala bora na mwengine mengi. jamaa kajitahidi sana. nawashangaa wanaojifanya vipofu wakati wao ndo wafaidika wakubwa.
kuhusu Magufuli ni mapema sana kumhukumu kwani ndo kwanza ana miezi michache tu tangia akalie ofisi. tumpe nafasi. akijipanga vizuri naye anaweza fanya vizuri au hata vizuri zaidi ya watangulizi wake.
 
Back
Top Bottom