Hakika siasa za Tanzania zimegubikwa na wingu zito lenye kiza kinene.Tangu awamu hii ya tano inayojipambanua ni serikali ya wanyonge iingie madarakani,tumeshuhudia uhuni mkubwa katika kile hawa wanasiasa uchwara wanaita "KUUNGA MKONO JUHUDI ZA BWN MKUBWA"!
Hiki ni kichekesho cha karne!Hivi kuunga mkono juhudi ni pale unapowasaliti wananchi walokuamini na kukupa kura kupitia chama ulichokuwemo!Wewe ni Meya,huwezi kuunga mkono juhudi kwa kusimamia vizuri mapato ya Halmashauri/Jiji,kuibua miradi mbalimbali,kuianzisha na kuisimamia kikamilifu?Ukifanya haya ukiwa katika chama chako utakuwa huungi mkono hizo juhudi?
Kituko kingine cha kitoto ni pale hawa wanaohama vyama wanapokuja na hoja mfu kwamba huko waliko " hakuna nia ya kweli ya kuwaletea maendeleo Wananchi,hakuna agenda ya maendeleo bali ni ugomvi"Huku ni kutufanya Watanzania hatunazo,haya mmeyajua leo?Mbona miaka yote hatukuwahi kusikia hizo ngonjera za kipuuzi mkiziimba?
Mi nadhani kama mnaamini wapinzani hawana agenda ya kuwaletea maendeleo wananchi,mnapotosha umma!Uthibitisho wa karibuni wa jinsi wapinzani walivo na uchungu na nchi hii ni juzi juzi tulimsikia Lema Godbless akimtahadharisha Mh Rais kuwa amezungukwa na wanafiki wanaobaki kumpigia pambio tu bila kumweleza ukweli!Siku kadhaa Mkata viuono akakutwa na kashfa nzito ilomwengua kwenye kiti chake pamoja na wenzie lukuki.
Lema alitanabaisha mengi sana.Wenye nia ya kweli na nchi hii ni wapinzani wanaotahadhalisha juu ya mambo mengi ya msingi lakini bado wanapuuzwa!
Lema huyuhuyu juzi amesikika akieleza msimamo wake juu ya waongoza watalii walioonesha ubovu wa barabara maeneo ya mbuga za wanyama.Kabla Mrisho Gambo alitaka vijana hawa wakamatwe na washtakiwe.
Kamanda Shana naye kwa kujipendekeza bila kufanya upembuzi yakinifu akalivalia njuga kichwakichwa. kwamba hao vijana pamoja na Lema siyo Wazalendo! Hahahahahaaaaaaa! Nyie ni watu wa ajabu kweli, kuwa mzalendo ni kuukana ukweli hata wa wazi!Kuficha ubovu wa barabara ndo uzalendo!Acheni kutufanya Watanzania wajinga!
Ajabu juzi Mh Kigwangala anawaombea msamaha vijana wale kwa Gambo!Msamaha kwa kosa gani wakati wameonesha uzalendo kwa nchi yao na sasa barabara zinatengenezwa?
Kama haitoshi,tumemsikia Mchungaji Msigwa akiishauri Wizara ya Maliasili na utalii juu ya njia bora za ku-attract watalii zaidi Mifano ipo mingi, mingi mingi kweli!
Leo mijitu michache kwa sababu ya tamaa na uroho wa vyeo ulojaa unafiki inaibuka eti wapinzani hawana agenda ya maendeleo ndo maana inahama! SHAME ON YOU!