Mnaohama vyama msifikiri Watanzania ni wajinga

Mnaohama vyama msifikiri Watanzania ni wajinga

Dragon Kulala

Member
Joined
Jan 24, 2020
Posts
53
Reaction score
80
Hakika siasa za Tanzania zimegubikwa na wingu zito lenye kiza kinene.Tangu awamu hii ya tano inayojipambanua ni serikali ya wanyonge iingie madarakani,tumeshuhudia uhuni mkubwa katika kile hawa wanasiasa uchwara wanaita "KUUNGA MKONO JUHUDI ZA BWN MKUBWA"!

Hiki ni kichekesho cha karne!Hivi kuunga mkono juhudi ni pale unapowasaliti wananchi walokuamini na kukupa kura kupitia chama ulichokuwemo!Wewe ni Meya,huwezi kuunga mkono juhudi kwa kusimamia vizuri mapato ya Halmashauri/Jiji,kuibua miradi mbalimbali,kuianzisha na kuisimamia kikamilifu?Ukifanya haya ukiwa katika chama chako utakuwa huungi mkono hizo juhudi?

Kituko kingine cha kitoto ni pale hawa wanaohama vyama wanapokuja na hoja mfu kwamba huko waliko " hakuna nia ya kweli ya kuwaletea maendeleo Wananchi,hakuna agenda ya maendeleo bali ni ugomvi"Huku ni kutufanya Watanzania hatunazo,haya mmeyajua leo?Mbona miaka yote hatukuwahi kusikia hizo ngonjera za kipuuzi mkiziimba?

Mi nadhani kama mnaamini wapinzani hawana agenda ya kuwaletea maendeleo wananchi,mnapotosha umma!Uthibitisho wa karibuni wa jinsi wapinzani walivo na uchungu na nchi hii ni juzi juzi tulimsikia Lema Godbless akimtahadharisha Mh Rais kuwa amezungukwa na wanafiki wanaobaki kumpigia pambio tu bila kumweleza ukweli!Siku kadhaa Mkata viuono akakutwa na kashfa nzito ilomwengua kwenye kiti chake pamoja na wenzie lukuki.

Lema alitanabaisha mengi sana.Wenye nia ya kweli na nchi hii ni wapinzani wanaotahadhalisha juu ya mambo mengi ya msingi lakini bado wanapuuzwa!

Lema huyuhuyu juzi amesikika akieleza msimamo wake juu ya waongoza watalii walioonesha ubovu wa barabara maeneo ya mbuga za wanyama.Kabla Mrisho Gambo alitaka vijana hawa wakamatwe na washtakiwe.

Kamanda Shana naye kwa kujipendekeza bila kufanya upembuzi yakinifu akalivalia njuga kichwakichwa. kwamba hao vijana pamoja na Lema siyo Wazalendo! Hahahahahaaaaaaa! Nyie ni watu wa ajabu kweli, kuwa mzalendo ni kuukana ukweli hata wa wazi!Kuficha ubovu wa barabara ndo uzalendo!Acheni kutufanya Watanzania wajinga!

Ajabu juzi Mh Kigwangala anawaombea msamaha vijana wale kwa Gambo!Msamaha kwa kosa gani wakati wameonesha uzalendo kwa nchi yao na sasa barabara zinatengenezwa?

Kama haitoshi,tumemsikia Mchungaji Msigwa akiishauri Wizara ya Maliasili na utalii juu ya njia bora za ku-attract watalii zaidi Mifano ipo mingi, mingi mingi kweli!

Leo mijitu michache kwa sababu ya tamaa na uroho wa vyeo ulojaa unafiki inaibuka eti wapinzani hawana agenda ya maendeleo ndo maana inahama! SHAME ON YOU!
 
Mwisho wa siku kila mtu ana uhuru wa kuhama chama iwe kwa sababu au hata pasipo sababu.

Kama kuna watu mnaumizwa na hii hamahama pelekeni bill bungeni.
 
Mwisho wa siku kila mtu ana uhuru wa kuhama chama iwe kwa sababu au hata pasipo sababu.

Kama kuna watu mnaumizwa na hii hamahama pelekeni bill bungeni.
Kuhama wahame lakini wasiwafanye wapiga kura wao ni wajinga kwa kutoa sababu za kipumbavu.

Hizo nafasi wanazotumia kujinufaisha wao binafsi Kwa kupokea hela haramu wajue wapiga kura wao walitoa jasho na damu hadi wakazipata, watu waliungua jua kupanga foleni kuwapigia kura, watu walikesha kulinda kura hizo leo wanabana pua eti wanaunga juhudi, huu ni utaahira.

Na CCM waelewe wapiga kura hao waliosalitiwa wamejenga chuki kubwa na chama hicho. Najua mnaringia mbeleko ya mabavu ya vyombo vya dola na wakurugenzi lakini mjue nao hao ni binadamu na wana utashi wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ndiyo pumbavu kabisa wewe naona hata std seven hukumaliza, unajua ulichokiandika? 10,000.

In God we Trust
Mkuu Mmawia! Tanzania haikuzoe kuwa na watu ambao akili yao haina Akili. Lakini tangu Mheshimiwa JPM aanze kuokota watu majararani watu wa aina hii wanaongezeka kwa kasi sana hapa Tanzania.
 
Kama yanayofanyika ni haki basi sawa , lakini kama si haki kwamba kuna hila na udhalimu nyuma yake basi tujue kuna Mungu mwenye Haki!

May God Almighty intervenes the situation soonest!


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom