Mnaodai kuwa Lissu amekosea kuhutubia kabla ya muda wa kampeni, siku ile Magufuli alikuwa ahutubii?

Joyce joyce

JF-Expert Member
May 23, 2020
457
1,973
Wakuu,

Nimeona watu kadhaa wakisema kuwaLissu amekosea kisheria kuhutubia wanachama wake kabla ya muda wa kampeni, najiuliza kuwa hawa watu kinewachanganya nini had kusahau kuwa Magufuli alihutubia baada ya kutoka kuchukua form tena akatumia vyombo vyote vya habari tena alikuwa akipiga kabisa kampeni, hivi siku ile si walifurahi na wakacheka?

Alikuwa akiwatukana wapinzani wake kuwa wabadilisha rangi au mmesahau? Know kinachowachanganya ni kilo? Si mlitamba siku ile mkaona kuwa mmeshinda? Hahahah Hahahaha Hahahaha

Hivi anaehutubia kwa kutumia TV tena live hotuba inaenda kwa Watanzania wote na anaehutubia watu walioko hapo hapo nani nani anafanya kampeni kati ya hao?

Siku ile mlikodi vyombo vya habari kuoneshwa nchi nzima mgombea wenu mkajiona wajanja, mkaona mmeshindaa? Na mkaona mmefunikaaa na mlitangaza kwenye vyombo vya habari mkutano ule nia ilikuwa muoneshe nyomi ya watu Wakati walikuwepo watu had toka mikoa mingne, mumemuona lisu amefunika tena Kwa idadi ya watu Wa kaeneo kale kale, kama nikijiji ni kutoka kijiji hicho hicho kama ni wilaya ni kutoka wilaya hiyo hiyo, mmepaniki

Hivi kwanini kila mnalolifanya kutaka kuonesha wapinzani kuwa mna watu, mnakubalika upinzani umekwisha linajibiwa kwa muda mfupi? Basi muwe mnakuwa wapole ndugu, tatizo mnashindwa kuelewa kuwa upinzani wa Watanzania uko kwenye damu
 
Hao jamaa pamoja na kuwa na dola lakini wa wivu Ile mbaya . Kwa akili zao walijua wakiwanunua wabunge na madiwani watakuwa wamemaliza kazi . Kumbe nafsi za watu zilingoja tu nani wa kuwaongoza na sasa Lissu amerudisha uhai.
 
Back
Top Bottom