Mnanishaurije kuhusu kuchukua cheti cha udereva NIT?

shadrackAmri

Member
Oct 27, 2023
5
3,144
Mimi nikijana niliehitimu mafunzo yaufundi mekaniks mwaka jana.

Mwaka huu nwezi wapili nikapata kazi nashukuru imenipa uzoefu mzuri sana kwenye masuala yaufundi

Lakini sasahivi ofisi imefilisika kiasi chasisi mafundi kukosa hela nimejalibu kuomba kazi sehemu kazaa nimekosa

Nimeweka hakiba yangu kama lakisaba hivi nafikiria nikajifunze udereva NIT ili niwe naomba kazi kotekote wakuu.mnanishaurije wakubwa kuhusu wazohili lakuchukua cheti chaudereva NIT?

nakama kuna mtu anajua gharama za kujifunza udereva NIT naomba anijuze na vigezo vyake ili nijiunge huko na nimuda gani hadi napata cheti.

Natanguliza shukrani wakuu
 
Inatakiwa kwanza uwe umesomea udereva sehem NIT awafundishi udereva wao wanatoa course za madereva whether unataka kusomea udereva wa kuendesha viongoz nk kwahyo kama ulishawah kusoma udereva sehem na una lesen nenda kaspecialize hapo hcho ndio ninachojua unaweza hata ingia kwenye Web yao au nenda chuo hapohapo ukaulize.
 
Lazima Uwe Na Leseni Hai, Isiyopungua Umri Wa Miaka Nadhani 5
Uwe Unajua Kuendesha Gari Vizuri, Aina Mbalimbali Unaweza Kupewa Tata
Ada Yao Sijajua Ila Haitapungua Laki 4.5
Lazima Uwapo Masomoni Ufauru Nadharia Na Vitendo
Usipofanya Vema Aidha Nadharia Ama Vitendo Utalazimika Kurudia Mtihani Huo Ndiyo Uweze Kupata Cheti.
 
Ha ha kwamba unaweza kupewa Tata uliendeshe. Hivi Tata ni gumu sana kuendesha mkuu?
 
Back
Top Bottom