Mnakumbuka jinsi wabunge wa CCM walivyokomaa kuhakikisha wakurugenzi wanakuwa maafisa wa Tume ya Uchaguzi?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,372
Nakumbuka kama si mwaka 2011 basi ni mwaka 2012 ambapo wabunge wa CCM walitumia wingi wao Bungeni kuhakikisha Wakurugenzi wa Halmashauri na watendaji wa kata wanaendelea kuwa ni Maafisa wa Tume ya Uchaguzi.

Kwa kumbukumbu zangu Bunge lilikuwa linafanyia marekebisho sheria ya uchaguzi ambapo wapinzani walikuwa wanapinga mapendekezo ya kuwatambua Wakurugenzi ama Wakuu wa wilaya kutambuliwa kama maafisa wa Tume ya Uchaguzi kwenye maeneo yao.

Nakumbuka mabishano yalikuwa makali ambapo baadhi ya wabungecwa CCM wakitaka wakuu wa wilaya wawe ndio wawe maafisa wa Tume na wengine wakitaka wakurugenzi wa Halmashauri ndio wawe maafisa wa Tume huku wapinzani wakipinga ama wakuu wa wilaya au wakurugenzi wa Halmashauri kutambuliwa na sheria kama wasimamizi wa uchaguzi katika maeneo yao pamoja na watendaji wa kata.

Hivyo ndugu zangu hii sheria ya uchaguzi ilitungwa kwa makusudi maalumu na ndio maana CCM walikataa tangu siku nyingi kuwaondoa wakurugenzi kwenye hii sheria na haya ndio matokeo yake.

Nakumbuka sana jinsi kina Mnyika,Lisssu na wabunge wengine wa upinzani walivyojaribu kujenga hoja lakini hoja zao zilikataliwwa na walio wengi.

Hakika wapinzani waliona mbali sana na wale wote ambao walikuwa wanawabeza na kuwakejeli wakati ule sasa watakuwa wanajionea aibu tu.

Sheria hij ya Uchaguzi imepitwa na wakati na hakika haifa kwa mfumo wa vyama vingi.
 
Nakumbuka kama si mwaka 2011 basi ni mwaka 2012 ambapo wabunge wa CCM walitumia wingi wao Bungeni kuhakikisha Wakurugenzi wa Halmashauri na watendaji wa kata wanaendelea kuwa ni maafisa wa Tume ya Uchaguzi.

Kwa kumbukumbu zangu Bunge lilikuwa linafanyia marekebisho sheria ya uchaguzi ambapo wapinzani walikuwa wanapinga Wakurugenzi na wakuu wa wilaya kutambuliwa na sheria kama maafisa wa Tume ya Uchaguzi kwenye maeneo yao.

Nakumbuka mabishano yalikuwa makali ambapo baadhi ya wabungecwa CCM wakitaka wakuu wa wilaya wawe ndio wawe maafisa wa Tume na wengine wakitaka wakurugenzi wa Halmashauri ndio wawe maafisa wa Tume huku wapinzani wakipinga ama wakuu wa wilaya au wakurugenzi wa Halmashauri kutambuliwa na sheria kama wasimamizi wa uchaguzi katika maeneo yao pamoja na watendaji wa kata.

Hivyo ndugu zangu hii sheria ya uchaguzi ilitungwa kwa makusudi maalumu na ndio maana CCM walikataa tangu siku nyingi kuwaondoa wakurugenzi kwenye hii sheria na haya ndio matokeo yake.

Nakumbuka sana jinsi kina Mnyika,Lisssu na wabunge wengine wa upinzani walivyojaribu kujenga hoja lakini hoja zao zilikataliwwa na walio wengi.

Hakika wapinzani waliona mbali sana na wale wote ambao walikuwa wanawabeza na kuwakejeli wakati ule sasa watakuwa wanajionea aibu tu.

Sheria hij ya Uchaguzi imepitwa na wakati na hakika haifa kwa mfumo wa vyama vingi.
CC: jingalao Lizaboni

Msitufanye wajinga.
 
Back
Top Bottom