Allelujah
JF-Expert Member
- Mar 9, 2017
- 452
- 414
Mzee mmoja alikuwa anachunga ng'ombe na mwanaye..wakati wanawarudisha Ng'ombe nyumbani..walikutana na mto..wale ng'ombe wakagoma kuvuka...mzee alitumia jitiada zake zote ila alishindwa..kwa hasira akawa anawachapa ng'ombe ila akuweza kuwavusha...Mara mtoto wake akamwambia Baba ukitaka wavuke..wewe tuwavushe ndama kwanza wakiona ndama wamevuka watawafuata ndama kwa nyuma..mzee alimsikiliza na walipowavusha ndama wale ng'ombe waliwafuata kwa nyuma...na ng'ombe wote walivuka..Ila Baada ya kuvuka kwa ng'ombe wote.."MZEE ALIAMUA KUMUUA MTOTO WAKE"..Unahisi ni kwa nini aliamua kumuua mwanaye wakati alimpa njia ya kuwavusha ng'ombe mtoni?