TANZIA Mmoja ya wamiliki wa mabasi ya Sumry, Humud Sumry afariki dunia

Aisee inawezekana kabisa mkuu
Nani aliwadanganya watu mafukara hawafi kwa korona? Matajiri ni maarufu ndiyo maana watu wana-share habari zao. Hivi unadhani muuza mchicha au dagaa anayekaa Yombo Vituka akifa kwa korona watu wa sehemu nyingine za nchi watafahamu? Sana watu wa karibu na mtaa anaoishi, ndugu, jamaa na marafiki ndiyo watapashana habari. Korona ipo na maskini wanakufa tena kushinda matajiri ila habari zao zinaishia huko huko wanakokaa. Hivi huyu anayejadiliwa hapa unadhani kama angekuwa dereva wa daladala tungejua?
 
Nilileta uzi kuwa Mungu anaisafisha dunia ule uzi nadhani uliwekwa kapuni.
Ila kwa ufupi ni kwamba Mungu anaisafisha dunia yake.
Kaa vizuri kijana usije kusafishwa
embu tuondolee porojo zako hapa. waliouweka kapuni huo uzi walifanya jambo la maana sana.
 
Aliyekuwa mmiliki wa mabasi ya Sumry, Humud Sumry, amefariki dunia Alfajiri ya leo Jumatatu Agosti 09, 2021 jijini Dar es Salaam.
Chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika na anatarajiwa kuzikwa leo jijini Dar es Salaam.

Nyepesi nyepesi nilizozisikia ni Corona alikuwa amekwenda Brazil kwa ajili ya vifaa vya ujenzi maana Humud yeye ni mkandarasi wa barabara na jioni hii hapa Sumbawanga tulikuwa na kisomo kwa ajili ya marehemu
 
Hii taarifa sijaielewa mwenye uelewe atoe ufafanuzi hasa watu wa sumbawanga wenye kuwajua vizuri..maana naona mitandao mingi inaandika salum humud summary na picha yake inaonekana.

Huyu salum sumry ni mtoto wa yule mzee sumry mmiliki wa mabasi toka kampuni inaanza. Maana nakumbuka mzee sumry alikuwa na watoto I think watatu mkubwa akiwa salum...Je anayezungumzwa na Ni salum au yule baba yake?
Aliekufa sio Salum aliekufa ni mdogo wake yule anajishughulisha na ujenzi wa barabara,madaraja nk
 
Walitisha sana kwa bus kali ila madereva waliwarudisha nyuma had familia ikaamua iwekeze kwenye kilimo
-1908935263.jpg
 
Back
Top Bottom