Mmmmmm!! Kaka hanielewi baada ya kuvunja ahadi

Asprin .................unaweza kuja shangaa ukiambiwa huyo Pretty bado anakula maisha kwa hela ya kaka!

kama kaka bado anahusika kwenye uchumi wa familia ya pretty na mumewe lazima atapata mdomo wa kusemea yote hayo.
 
Ushauri mzuri. Ila BJ kwa usalama wa baioloji yangu na usalama wa hawa mabinti hapa kibaruani na kwa ajili ya ufanisi mzuri wa kazi na kwa ajili ya usalawa wa screen ya kompyuta yangu, nakuomba kwa nia njema kabisa uibadili hiyo avatar yako.

Tafadhali Tafadhali Tafadhali:focus:

Hee Asprin umenishtua, usije kusababisha matatizo hapa!..Haya, your wish is my command, only kwa avatar ha ha...

Haya, back to kaka mwenye wivu!..
 
Ufafanuzi zaidi tafadhari

kwa sasa ni nani anahudumia, analipa tuition fees n.k

Kama ni kaka lazima imuume, alitegemea umalize ujitegemee ndipo uolewe.
Otherwise ataelewa kadri siku zinavyosonga.
 
Kaka anamaanisha.. hana wivu.. anamtakia mema my sister wake.. Jaribu kumsihi na kumwomba radhi ya kuwa hukutegemea kuipata hy mimba.. ni bahati mbaya tu.
 
pole sana pretty, just give ur brother some time atakuzoea tu katika hali hiyo muhimu muonyeshe you can handle both of them, yani ujauzito wako hautaaffect performance yako kielimu.
inakua ngumu kwake kukubali kutokana na kwamba bado ana fikra kwamba u are still his young baby sister anapenda bado kukuongoza kwenye mafanikio, huyo kaka hana nia mbaya kabisa nawe its just he love her sister sana! u are lucky to have a brother who care pretty!
...Huenda bro roho inamuuma anapoona sister ana ujauzito maana yake kuwa kuna njemba limefanya mambos...upendo mwigine mtu anatamani dada yake asiguswe kabisa...ndio huyo kakaye!!
 
........Hello wana JF
Mwenzenu simuelewi my bro, kipindi nilivyotaka kuolewa alipinga sana kwa kigezo bado nasoma japokuwa mie sikuona tatizo lolote kwa elimu ninayosoma haipo ngumu sana hadi nishindwe kuolewa kwa sababu ya masomo............kaka alipinga sana na kutaka nije kuolewa baada ya kumaliza masomo yangu, lakini wazazi hawakuwa na pingamizi maana waliona nimeshajikomalia zangu hivyo naweza kumudu mikiki ya ndoa na masomo.

.......Baada ya muda alivyoona nimekomalia kuingia ndoani akaamua kukubali lakini kwa masharti........aliniambia kwamba nisipate ujauzito hadi nimalize masomo, nami nikamuhakikishia kwamba nitajitahidi nisishike mimba hadi nimalize chuo,,, lakini sasa Mungu alivyo wa ajabu baada ya miezi 2 ya ndoa mie nikanasa mimba.........hivi sasa nipo likizo nimerudi home, hivyo ikabidi nikamjulie hali kaka yangu mpendwa nyumbani kwake,lakini cha ajabu baada ya kuona hali niliyokuwa nayo ya ujauzito kaka kakasirika hakuwa na furaha. Nakwambia nimesemwa mie na kaka hadi basi..........mbaya zaidi kaamua kunichunia sababu nimevunja promise.Hajui sasa mie sio mtoto tena nina ndoa yangu hivyo nimekuwa mtu mzima.

..........Kwanza ni kaka yangu pekee ninampenda na yeye alikuwa ananipenda na kuniongoza vizuri haswa kielimu.
Mwenzenu sijui nifanyeje?.........I mean nitumie mbinu gani ili nielewane na kaka yangu maana nampenda sana kaka yangu sipendi kuona anakasirika kwa ajili yangu.

Pole sana Mrembo, mikaka mingine ndivyo ilivyo. Hajui hayo anayoyafanya yanaweza kabisa kuchangia matatizo kwenye ujauzito wako. Kama bado hataki kukuelewa kwamba wewe ni mtu mzima sasa na unaweza kufanya maamuzi yako bila ya kuingiliwa na yeyote, basi jaribu kumuepuka mpaka utakapojifungua ili kuepusha matatizo katika ujauzito wako. Kila la heri.
 
........Hello wana JF
Mwenzenu simuelewi my bro, kipindi nilivyotaka kuolewa alipinga sana kwa kigezo bado nasoma japokuwa mie sikuona tatizo lolote kwa elimu ninayosoma haipo ngumu sana hadi nishindwe kuolewa kwa sababu ya masomo............kaka alipinga sana na kutaka nije kuolewa baada ya kumaliza masomo yangu, lakini wazazi hawakuwa na pingamizi maana waliona nimeshajikomalia zangu hivyo naweza kumudu mikiki ya ndoa na masomo.

.......Baada ya muda alivyoona nimekomalia kuingia ndoani akaamua kukubali lakini kwa masharti........aliniambia kwamba nisipate ujauzito hadi nimalize masomo, nami nikamuhakikishia kwamba nitajitahidi nisishike mimba hadi nimalize chuo,,, lakini sasa Mungu alivyo wa ajabu baada ya miezi 2 ya ndoa mie nikanasa mimba.........hivi sasa nipo likizo nimerudi home, hivyo ikabidi nikamjulie hali kaka yangu mpendwa nyumbani kwake,lakini cha ajabu baada ya kuona hali niliyokuwa nayo ya ujauzito kaka kakasirika hakuwa na furaha. Nakwambia nimesemwa mie na kaka hadi basi..........mbaya zaidi kaamua kunichunia sababu nimevunja promise.Hajui sasa mie sio mtoto tena nina ndoa yangu hivyo nimekuwa mtu mzima.

..........Kwanza ni kaka yangu pekee ninampenda na yeye alikuwa ananipenda na kuniongoza vizuri haswa kielimu.
Mwenzenu sijui nifanyeje?.........I mean nitumie mbinu gani ili nielewane na kaka yangu maana nampenda sana kaka yangu sipendi kuona anakasirika kwa ajili yangu.
Inavyosomeka bro ana aleji na mimba na anawachukia watoto . Pia inaonekana hapendi majukumu kabisa. Unapomtembelea wewe msifie mumeo na tena kilichotokea jana yake kuwa mtanunua gari na bwana wangu kapanda cheo mpe story uone kama atamsifia unayempenda.
 
ulishawahi kuongea nae kinagaubaga juu ya hilo? yawezekana alikuwa na malengo mazuri sana na wewe hapo baadae. anyway umeishaolewa tunategemea uwe na independent thinking whether utamuuzi kaka au nani unachokiangalia ni familia yako na furaha ya ndoa yako.
 
Back
Top Bottom