Mmiliki wa mabasi ya Zakaria amenidhulumu mali yangu na kutishia kuniua

Traffic atakayesimamisha hizo gari huwa anafuatiliwa sana, madereva hawapati shida sana hata gari ikiwa na kosa wakikamatwa wao ni kumjuza bosi wao haraka......na bosi ana respond immediate baada ya mda mfupi huachiwa safari ieñdelee...nasikia huyo jamaa alikuwa jambazi aliyeshindikana kipindi cha nyuma kwahiyo kila mtu anamfahamu vizuri tu huyo. Pole sana mtoa mada, akusamehe akurudishie kamzigo kako
 
Siku Ya Kwanza Binadam kuoga aliogeshwa pia siku ya mwisho itakuwa hivyo hivyo haijalishi una nini utaogeshwa tu.

Dhulumati haifai
 
wachangiaji kama nyie wa akina the last don umu huwa hatuwataki, inamaana k
ilo gar lote lilibeba mizigo mpaka achukue mizigo yote? inaskitisha tupo majukwaan na watu wasiojielewa, mtu kadhurumiwa haki yaki tunaacha kumpigania apate haki yake tunaanza taarabu tena! hv ww the last don ulishawah kusafir? na kama ulishawah kusafir ulibeba biashara gan kama sio kibegi tu cha mgongon chenye surual moja, sasa kama ww ulisafir na kisuruali kimoja ina maana ndan ya gar wapo na wengine kama ww kwa iyo ulitaka uyo apitie na iko kisurual chako kimoja ndio uamin kama na uyu kaibiwa viatu vyake? mwizi anaangalia fursa na ndio maana kaamua kuchukua viroba vya viatu
 
Siku nyingine uwe na kijisimu chenye uwezo wa kurekodi sayti mfukoni.. atleast uwe na ushahidi wa kushikilizia maneno yako
 
......kwanini hakukiuka kama yeye mwanaume hasa,haambiwi kitu na mtu!??
..anaonea dagaa na kuna watu anakula nao,sio!??
Yeah......hiyo ipo pote.....kwani si hata Pogba kuna watu kibao kawashindwa anahangaika na vidagaa tu?
 
Hapana sio sahih kuwa vyombo vya dola wameshindwa hilo mim nakataa suala ni kwenda kituo cha police cha karibu fungua kesi vifuatavyo ni muhim ktk kufungua kwako kesi list za mzigo,list ya kulipia mzigo wakat wa kuusafilisha, wakati yeye anakufuata kuueleza kuwa mzigo atauchukua kwa kuwa utaunguza gar wew ulikuwa na akina nan, je dereva na kondakta wako wanatambua mgogogoro huo pia mwisho fungua kesi hakuna MTU/tajir aliye juu ya JINAI(CPA) na KATIBA pia mkoa wa Mara unamakamanda watenda haki wasioogopa Hata kidogo nenda ofic ya RCO musoma nb angalia ucje kuleta siasa kwenye mambo muhim ukaaribu majina ya watu ni vibaya
 
Ni Yule tajiri wa mabasi ya Zakaria yanayotoka Mwanza hadi Silari mpakani mwa Kenya, na kada mkubwa wa chama cha mapinduzi (ccm).

Wiki tatu zilizopita nilinunua mzigo wa viatu kutoka Kenya na nilikuwa na vibali vyote vinavyoniruhusu kufanya biashara bila Shaka yoyote.

Kwa miaka mingi nimekuwa mteja wa mabasi ya Zakaria, uteja wangu ukahitimishwa wiki tatu zilizopita baada ya Zakaria mwenyewe tajiri wa mabasi hayo kanifuata stendi ya Tarime akiwa kaongozana na mfanyakazi wake mmoja turn boy wa mabasi yake na kisha kunipora mzigo wangu wa viatu wenye thamani ya sh 2,800,000.

Akidai kuwa mzigo huo ungekaa kwenye buti la basi yake ungeiunguza hiyo gari yake.
Nilishangaa Sana, ni mara nyingi Sana nimekuwa naweka viatu kwenye buti lakini hakuna basi lililowahi kuungua.

Nilidhani ni masihara kumbe ni kweli Zakaria alikuwa amedhamiria kunipora mzigo wangu.

Niliteseka Sana kupata mtaji leo hii mtu ambaye tayari kashatajirika ananidhulumu viatu vyangu vya biashara bila aibu yoyote.

Nilimfuata kumbembeleza Zakaria anipatie mzigo wangu akaniambia kuwa Nikiendelea kumsumbua atavichoma moto viatu vyangu.

Sikuishia hapo, nilimfuata padri wa kanisa lake ili ambembeleze Zakaria anirushie mzigo wangu lakini haikuwezekana.

Nikamfuata tena rafiki yake Gachuma ili amsihi anirudishie mzigo wangu lakini pia haikuwezekana kabisa.

Nikaamua kwenda police, huko ndo nilichoka kabisa ,Police waliniambia wao hawamuwezi Zakaria, inatakiwa nirudi tu kumbembeleza, niliporudi kumbembeleza Zakaria akanionya nisijaribu tena kumfuatafuata maana atanipiga risasi.

Mali yangu mwenyewe natishiwa kuuawa bila? Au ni Kwa Sababu Zakaria ni kada Wa chama dola?
6e07f7addf3fd8e2f5e627e2f40af75b.jpg

Nimeambiwa mimi siyo wa kwanza kuporwa mali na Zakaria, ni wengi sana wameporwa ila tu Hawana pa kusemea, hadi Nimeamua kuja humu kutoa malalamiko yangu na jinsi maisha yangu yalivyo hatarini endapo tu nitaendelea kudai haki yangu, ni kwamba imeshindikana kabisa kila njia kupewa mzigo wangu na tajiri Zakaria.

Ni Kwa Sababu ya utajiri wake ndo aninyime haki yangu na kutaka Kuniua?
Nataka nimwambie Zakaria kuwa, haya ni maisha tu, asidhani atakuwa juu Siku zote, yuko wapi J4 na mabasi yake? Yuko wapi Ndugu?

Zakaria kula huo mzigo ila Mungu yupo atanilipia, jasho la mnyonge huwa haliendi bure, sikuwahi kufikiria Kama Zakaria ni mtu wa aina hii.
mkuu hakikisha unachokisema kipo sahihi maana kesi ya kumchafua mtu mkubwa kama yule ni kubwa, ndo litakuwa fundisho maana utauza hadi godoro kulipa. Isitoshe hapa umelichafua jeshi la polisi na CCM. Nakuonea huruma sana.
 
Faru Yohana
Hongera Kwa kutoa yako ya moyoni Kwa wanaJF.Mada imepoteza msisitizo kwa sababu ya kuingiza UCHAMA katika swala muhimu la dhulma na uonevu.Wengi wetu humu ni makada wa vyama tofauti Kwa hiyo maoni yetu yatakuwa kichama sio Kwa dhulma na uonevu wa huyo "mungu mtu".
Swali dogo la nyongeza Mh Faru Yohana
Kwa nini hujaeleza upande wa huyo aliyekudhulumu mali yako? Ni vigumu kuamini udhulumiwe Na sababu ulio itowa hairidhishi.
Ukiwa umelipia mzigo wako wa halali nategemea risiti unazo? Wanasheria wataweza kukusaidia kwa kiwango kidogo cha fedha Na ukishinda kesi utalipwa fidia ya usumbufu wako.
 
Mkuu hebu weka mambo vizuri hapa! Yaani Zakaria atoke huko atokako aje akamate mzigo wako tu bila sababu? Kuna taarifa umezificha mkuu! Kwani kutoka huko Kenya ulikuwa umepakiza kwenye basi lake? Au ulikataa kulipa nauli uliyokuwa umeambiwa ndo maana jamaa akaja anasema huo mzigo ungeunguza basi lake? Weka taarifa zote hapa usikimbilie huruma ya wana-JF!
 
Miaka ya 90 mwishoni, Peter Zakaria ilisemekana ni mafia wa hatari. Siku zile mabasi yake yalihusishwa na usafirishaji wa bangi kutoka Tarime hadi Mwanza.
Nakumbuka miaka ile palikua na ushindani mkubwa wa kibiashara ulio pelekea uhasama mkubwa kwa mabasi ya Zakaria na Bunda Bus, hii ilikua uhasama kuanzia wamiliki wa mabasi, madereva hadi makondakta.
Nakumbuka miaka ile ya 90 kuelekea mwishoni, kuna dereva wa bus la Bunda alimwagiwa tindi kali kutokana na umahiri wake wa kuendesha basi kwa mwendo kasi na ustadi mkubwa na kuishinda Zakaria kila wanapo ondoka pamoja. Sakata lile ilisemekena Peter Zakaria alihusika pia nakumbuka hata ushahidi ulipatikana na hatima nakumbuka Peter Zakaria alimlipa dereva yule pesa nyingi na akamfidia kwa kumpa moja kati ya mabasi yake.
Tukiwa kwenye maongezi tukimjadili tajiti mwingine m-babe (Kitana) na pia ilisemekena pia anajihusisha na ujambazi, uporaji kwa wavuvi ndani ya ziwa victoria
Miaka ya 2000 kuelekea mwishoni nilisikia kwamba Peter Zakaria ameamua kurudia Mungu na kumtumikia, na nilisikia alirejea na akawa mtu mwema sana.
upo sahihi mkuu, Zakaria alishaokoka na kumrudia Mungu wake, hachapi viboko tena watu, mleta mada ni mchonganishi tu.
 
Hajasema amenyang'anywa mzigo wake kwa sababu gani? alishindwa kulipia gharama za usafirishaji au vp? kutafuta huruma tu humu hakusaidii km usiposema chanzo cha mgogoro wenu na Zakaria, ukizingatia huyo jamaa hapo kanda maalum sidhani km kuna askari anaweza hata kukamata bus lake achilia mbali kumkamata yy kwa kosa lolote.
 
Kk umezulumiwa mzgo mkubwa sana In Shaa Allah Allah atakulpia hapa hapa dunian kama kwel n jasho lako na maneno uliongea n kwel bas Allah atakuhukumia hap hapa
 
Back
Top Bottom