Faru Yohana
New Member
- Dec 31, 2016
- 4
- 58
Ni Yule tajiri wa mabasi ya Zakaria yanayotoka Mwanza hadi Silari mpakani mwa Kenya, na kada mkubwa wa chama cha mapinduzi (ccm).
Wiki tatu zilizopita nilinunua mzigo wa viatu kutoka Kenya na nilikuwa na vibali vyote vinavyoniruhusu kufanya biashara bila Shaka yoyote.
Kwa miaka mingi nimekuwa mteja wa mabasi ya Zakaria, uteja wangu ukahitimishwa wiki tatu zilizopita baada ya Zakaria mwenyewe tajiri wa mabasi hayo kanifuata stendi ya Tarime akiwa kaongozana na mfanyakazi wake mmoja turn boy wa mabasi yake na kisha kunipora mzigo wangu wa viatu wenye thamani ya sh 2,800,000.
Akidai kuwa mzigo huo ungekaa kwenye buti la basi yake ungeiunguza hiyo gari yake.
Nilishangaa Sana, ni mara nyingi Sana nimekuwa naweka viatu kwenye buti lakini hakuna basi lililowahi kuungua.
Nilidhani ni masihara kumbe ni kweli Zakaria alikuwa amedhamiria kunipora mzigo wangu.
Niliteseka Sana kupata mtaji leo hii mtu ambaye tayari kashatajirika ananidhulumu viatu vyangu vya biashara bila aibu yoyote.
Nilimfuata kumbembeleza Zakaria anipatie mzigo wangu akaniambia kuwa Nikiendelea kumsumbua atavichoma moto viatu vyangu.
Sikuishia hapo, nilimfuata padri wa kanisa lake ili ambembeleze Zakaria anirushie mzigo wangu lakini haikuwezekana.
Nikamfuata tena rafiki yake Gachuma ili amsihi anirudishie mzigo wangu lakini pia haikuwezekana kabisa.
Nikaamua kwenda police, huko ndo nilichoka kabisa ,Police waliniambia wao hawamuwezi Zakaria, inatakiwa nirudi tu kumbembeleza, niliporudi kumbembeleza Zakaria akanionya nisijaribu tena kumfuatafuata maana atanipiga risasi.
Mali yangu mwenyewe natishiwa kuuawa bila? Au ni Kwa Sababu Zakaria ni kada Wa chama dola?
Nimeambiwa mimi siyo wa kwanza kuporwa mali na Zakaria, ni wengi sana wameporwa ila tu Hawana pa kusemea, hadi Nimeamua kuja humu kutoa malalamiko yangu na jinsi maisha yangu yalivyo hatarini endapo tu nitaendelea kudai haki yangu, ni kwamba imeshindikana kabisa kila njia kupewa mzigo wangu na tajiri Zakaria.
Ni Kwa Sababu ya utajiri wake ndo aninyime haki yangu na kutaka Kuniua?
Nataka nimwambie Zakaria kuwa, haya ni maisha tu, asidhani atakuwa juu Siku zote, yuko wapi J4 na mabasi yake? Yuko wapi Ndugu?
Zakaria kula huo mzigo ila Mungu yupo atanilipia, jasho la mnyonge huwa haliendi bure, sikuwahi kufikiria Kama Zakaria ni mtu wa aina hii.