Hakuna nchi yenye hati miliki,ila kiswahili cha unguja yaani KIUNGUJA NDIO kilitambuliwa kimataifa kama kiswahili huku kile cha kenya kikiachwa na kama sikosei mana kumbukumbu zangu ziko mbali ni KIMVITA(cha kenya).
KIMVITA na KIUNGUJA ndizo lahaja mbili zilikuwa zimekubalika zaidi na zilileta vita ni lahaja ipi itambulike kama lugha ya kiswahili,na kwa tetesi nilizonazo ni kwamba baada ya haki ya kiswahili kwenda kwa lahaja ya KIUNGUJA huku KIMVITA kikiachwa kenya ilikasirika na kuamua kuifanya lugha ya taifa kuwa KIINGELEZA lakini ilikuwa lugha ya taifa iwe kiswahili kama tanzania.
SO KENYA INA HISTORIA KUBWA PIA KATIKA KISWAHILI sema tofauti wao lahaja yao iliyokuwa ikipigiwa upatu haikuchaguliwa.
IKUMBUKWE pia kuwa kulikuwa na lahaja nyingi sana za kiswahili katika mwambao wote wa pwani ya bahari ya hindi ukianzia tanganyika,kenya,somalia,ethiopia.LAKINI kimvita na kiunguja ndizo lahaja zilizoonekana bora kupewa utambulisho wa kiswahili