Kwa muda mrefu nilikuwa naiona hii kampuni ya interchick inakua mpaka kufikia leo hii... Sasa hapa jamvini watu wengi wana plans za kufuga kuku na mayai na vifaranga
Hapa mjini wa akina mama wengi wanafanya biashara ya kuku wa nyama na mayai ila ukiangalia kwa undani biashara hii imekuwa kama second option yaani katika familia mke wa nyumbani ndio anasaidia kuingiza kipato cha nyumbani as second option ila first option ni shuguli anazofanya mzee (sijui mmenielewa hapa)
Ila kwanini kuku isiwe the first business kwanini kuku isiwe biashara ya kwanza ambayo mtu anaingiza na ikamfanya awe bilionaire??
Mfano interchick.
Je kuna mtu yeyote anajua jinsi jamaa mwenye interchick alivyoanza??
Jinsi alivyoendesha biashara yake
Na mmiliki wake profile kiujumla
Natanguliza shukrani
mkuu ... kwa sasa hivi mmiliki wa INTERCHICK ni kampuni tanzu ya KENCHICK ya Kenya ....
Watanzania sisi wa ngozi nyeusi inakuwa ngumu kufikia level hizo kwakuwa haya mambo ni magumu kufanya mtu peke yako kama individual hadi muunganishe nguvu muwe 2 ,3 ,5,10 nk . Sasa sisi tukishakuwa watu wengi lazima kutatokea kutokuelewana ndio maana kila mtu anafanya kidogo kidogo. Juzi niliangalia Habari TBC nikaona jamaa wameunganisha nguvu huko Bukoba wanafanya ufugaji mkubwa wa ng'ombe mafanikio waliyopata kwa kweli its amazing!!!
Mtindo wa kuunganisha nguvu ndio njia mbadala kwa wenye mitaji kidogo,la msingi ni kupata timu nzuri.
Kweli, kilimo ndo mpango mzima.Na kupata timu nzuri ndo ishu ilipo mkuu ila fursa ni nyingi sana na kuna mwanga mbele katika kilimo na ufugaji