YoungCorporate
JF-Expert Member
- Apr 30, 2010
- 391
- 113
Nadhani labda swali la msingi ni je utolewaji wa bure utakuwa wa quality ipi? Kimsing sioni tofauti yeyote itakayotokea ukilinganisha na sasa, na sidhani kama kuitoa bure kutatupeleka mbele. Kwa sasa shule ya msingi ni bure na sekondari ni elfu 20 mpaka 70 (mnaojua mnisahihishe). Hii ni gharama ndogo ambayo yaweza kufutwa tu bila shida.
Chuoni pia kunatolewa mikopo ambapo urejeshaji wake unalegalega kwa hivo ni kama nusu bure kwa wanopata mikopo. Kwa maana hiyo kitakachofanyika ni kufuta hizo za sekondari na kutodai marejesho chuo kikuu baada ya wahatimu kupata kazi, ambayo sidhani kama ni sera endelevu na itachangia kupunguza uwezo wa bodi kutoa hizo upkeep fees.
Najua hili ni suala la kisiasa zaidi pengine wenye sera hii watupe manufaa ya kuifanya elimu kuwa bure?? Kwa mtazamo wangu maboresho ya elimu inayotelewa kwa maana ya quality, mtaala, walimu, majengo, maabara, ni muhimu zaidi kuliko kuifanya bure.
happy sunday