Mmh !! Nimemaliza mtihani wa kwanza ila huu sasa !!

Duu mkuu kama ulishamwambia jinsi mama yako alivyo kabla hujamuoa alafu akakubaliana na hiyo hali alafu baada ya ndoa anjifanya kugeuka..huyo simke hakufai ushamweleza madhaifu ya mama yako hapo kabla ya ndoa akakubali kuishi nae ndani ya madhaifu yake leo anabadilika huyo acha alitaka ndoa sio maisha
 
Ikiwa mkeo haelewani na mama yako, huyo sio mke wakukaa nae...
 
Nunua zawadi na kumpa mke wako ampe mama...kikifanyika kitu kizuri kwa mama muweke mkeo mbele aonekane yeye ndo kamfanyia...watengenezee mazingira...wamama huwa wanapenda antention ya watoto wao wa kiume..akiona unamjali zaidi atampenda mke wako
 
Ukishindwa kutatua mgogoro wa mke wako na mamako bado wewe mvulana !!!karibu chama chetu Cha ubachelor.mama ako umekanae muda mrefu ukishindwa kujua tabia yake ili uoe mwanamke anayeweza kuendana na tabia yake .mfano mimi familia yetu ni wachawi lazima nioe mchawi ili tuoane kivyote ,Mambo popompo Kama haya ndio badae yanaleta mchwererere kwenye familia.
Duu!
 
Hamuishi pamoja lakini migogoro haiishi. Uende kumtembelea mama yako pekee yako na mara chache sana unakwenda na familia hata mama yako apunguze kufika kwako yote hayo kupunguza ugomvi. Wanawake wakiwa pamoja hawaachi kugombana
atakuwa bado anamtegemea mamake, sasa mke kaolewa na mabwana wawili,
 
Mkuu, mama yake apunguze kufika kwake means jamaa ampangie ratiba kwamb mama inabidi uje kwangu baada ya mda flan? Mbona hiyo ngumu tena hapo ungomvi ndo utakuwa mkubwa zaidi.
Hamuishi pamoja lakini migogoro haiishi. Uende kumtembelea mama yako pekee yako na mara chache sana unakwenda na familia hata mama yako apunguze kufika kwako yote hayo kupunguza ugomvi. Wanawake wakiwa pamoja hawaachi kugombana
 
Asante cna, sehemu anapkaa Mama Yangu unapanda dala dala kufka Huko na mimi Ndio Niko karibu na Mama yangu Ndugu zangu wengine wapo nje Ya mkoa huu. Hivyo mara nyingi mimi Ndio Nategemewa kwenda kumsabahi mara moja moja ukizingatia ni mjane
Mtaftie kiben10 kama ni mjane
 
Ukweli mama yangu ni muongeaji cna na ni mtu wa fact yaani yeye hapindishi ukweli ni ukweli na sisi tumelelewa hivyo nakumbuka kipindi cha uchumba kuna kipindi Wife alipitiwa kidogo mama alimuita na kumkanya waziwazi basi toka kipindi hicho mke hamkubali kabsa nilishawahi kumwambia toka cjamuoa kuwa mama yangu yuko Hivi Akasema Sawa nitaweza kukaa nae maana yeye hakopeshi na tena nilishawahi kumkanya na kumwambia mama yangu Huyu ni Mjane na mimi Ndio Niko karibu nae mkoa huu kumuangalia naomba umvumilie naona mziki ni ule ule tu tena ukimwambia Ndio anakumbushia yale ya nyuma
Anakumbushia ya nyuma yapi ungeyaweka waz ila inaonekana mkeo kumbe ndo anamakosa kwa hayo maelezo yako.
 
Habarini !! Tayari nilifanikiwa kupata mke miaka miwili sasa na mtoto juu, ila Mke na Mama yangu hawaelewani kila cku maneno mke hamsikilizi mama kwa chochote ukifka kwa mama naye malalamiko, nilishawahi kumkanya Kidogo mke kuwa mvumilivu na Mama yangu lakini imeonekana kuwa ngumu, ingawa hatukai karibu na Mama yangu ila mkoa ni mmoja bado inakuwa issue, Embu nishaurini wale walio kwenye ndoa huu Mgogoro utaisha kweli !? Maana mke namtaka Mama namtaka
Tatizo ni kwamba hapo katika msebule wako panang'aa sanaa kuliko kwa mama mzazi,, pendezesha pia kwa mama mzazi,,,

Badirisha zile sofa kaka,, pia mpe mtaji mama mzazi., aingize kipato chake, pia mke mpe mtaji wake,

Changamoto ndo maisha
 
kwa hiyo ndo maisha hayo, maana kipindi cha nyuma kuna Mzee mmoja aliwahi kuniambia hao kuna kitu wanagombania sasa cjui Nini mpaka leo Cjajua
Hao wanakugombea ww.Mzee wangu alishanambia kuwa inapofika muda mtoto wa kiume anaoa huwa kama mzazi hasa mama anapaswa na analazimika kukuachia toka kwenye moyo wake na akubal kuwa sasa hana tena umiliki juu yako zaid ya upendo wa mtoto na mzazi.
Akina mama huwa wana fail sana hapa.Othwerwise kama awe amegundua jambo baya juu ya mkeo na haatak kukuambia.

Vinginevyo mother akubal tu kuwa it will never be the same baina yake na ww.akuache na maisha yako.
 
Habarini !! Tayari nilifanikiwa kupata mke miaka miwili sasa na mtoto juu, ila Mke na Mama yangu hawaelewani kila cku maneno mke hamsikilizi mama kwa chochote ukifka kwa mama naye malalamiko, nilishawahi kumkanya Kidogo mke kuwa mvumilivu na Mama yangu lakini imeonekana kuwa ngumu, ingawa hatukai karibu na Mama yangu ila mkoa ni mmoja bado inakuwa issue, Embu nishaurini wale walio kwenye ndoa huu Mgogoro utaisha kweli !? Maana mke namtaka Mama namtaka
WEWEendelea na mkeo kumwambia asijibizane na mama yako. Kama mnaishi mbali ugomvi unatoka wapi? Yawezekana kabisa mama yako kuna jambo baya la huyo mkeo ambalo ni vigumu kukueleza sasa kwa kuwa amekuwa akikulinda toka u mtoto huwa mara nyingi wanaamini kwa huo wajibu hata ukiwa mkubwa. NI JUU YAKO KUMCHOKOZA MAMA AKUELEZE ILA NGUMU. Naielewa hii km kama mchepukaji ni rahisi mama yako kulijua hilo mapema sana na kumchukia mkeo kuwa anakuangamiza.
 
Mimi huwa Nina msimamo mmoja.
Mama yangu Ni mmoja tu na Wala hawezi kutokea mwingine.
Mke yeyote anaweza kuwa Kati ya Hawa waliojaa humu barabarani.
Wengine wanatamani hata kutamkiwa tu kuwa wanaolewa na hawapati nafasi hiyo.!!
Mke akishindwa kuendana na mama yangu hata kinafiki hawezi kuendana na Mimi.
Mama yangu ndiye aliyenifanya nikawa vile amenikuta na ndevu kibao.
Pamoja na ukorofi wake, ulevi, uchoyo, uchawi nk lazima aheshimu kuwa ndio mama yangu.!!
Mambo ya kumtesa mama yangu aafu mama yake ndio anataka aheshimiwe ni ujinga.!!
Kikubwa Ni kuishi mbali na familia ya mzee wako ujitegemee ili wasiwe karibu.
Lakini Upendo kwa mama yako usipungue.
Bila mama yako usingekuwa duniani lakini bila huyo mke maisha yanadunda tu kama kawaida.!!
Mke Ni rafiki wa muda tu.
 
Suluhu ya tatizo ni kukaa nao wote wawili kwa pamoja na uanze kuhoji kila mmoja ana tatizo gani. (Mwanaume aliyekamilika tu ndo ataweza kuendesha hichi kikao) usikilize kila upande na ufanye mamuzi bila kuegemea upande wowote...

Likishindikana hilo basi hamieni mkoa mwingine kabisa, muwe mnaonana mara moja kwa mwaka hakutakuwa na ugomvi
Mkuu hata Kama mama ana makosa mke anatakiwa kutambua kuwa Ni sawa na mama yake!!
Kwani mama yake akikosea huwa wanakosana?
Yaani nimuite mama nimdhalilishe mbele ya mwanamke tuliyekutana ukubwani aanze kueleza hisia zake?
Kwamba anaona wivu ninavyomnunulia mke nguo nzuri??
Huyo mke akijua hayo ndio ataanza kumpenda?
Kama sio ataanza kumtangaza kwa ndugu zake!!!
 
Mkuu hata Kama mama ana makosa mke anatakiwa kutambua kuwa Ni sawa na mama yake!!
Kwani mama yake akikosea huwa wanakosana?
Yaani nimuite mama nimdhalilishe mbele ya mwanamke tuliyekutana ukubwani aanze kueleza hisia zake?
Kwamba anaona wivu ninavyomnunulia mke nguo nzuri??
Huyo mke akijua hayo ndio ataanza kumpenda?
Kama sio ataanza kumtangaza kwa ndugu zake!!!
Kuwaita pamoja ni kumdhalilisha mama?

Kama unajua mama yako anamuonea wivu mkeo ukimnunulia nguo mpya kwa nini na yeye usimnunulie kuepuka tatizo?

Umeomba ushauri na mimi nimetoa kama wengine walivyotoa, sio lazima uuchukue kama unaona haukufai uache mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom