Mmh mapenzii bhasiii tena...

batmanwafez

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
882
1,341
Habarini wanajamii wenzangu. Nahisi hii itakua post yangu ya kwanza upande huu adimu wa malove love...
Anyway twende moja kwa moja ndani.
Mim ni kijana nipo mid 20s kwahio sio mzee sanaa.
Mwaka jana kwenye mwezi wa kumi hivi kuna jamaa tupo nae kazini pale akaja na kabinti. Mh kasichana kazuri zuri hivi, mim hapo hapo kakawa kameshika attention yangu.
Sasa baada ya kale kabinti kuondoka...kwenye maongezi yetu na jamaa nikachomekea kumuuliza jamaa kuhusu hako kabinti.
Jamaa akaniambia ni mdogo wake ila hawako related sanaaa...ila wanaitana kaka na dada. Halafu pia akaniambia kwamba kapo single.
Enhh mim kusikia hivyo nikapiga vigelegele...yani furaha sio ya dunia hii.
Bhas nikwambia kimatani akalete siku nyingine....maana mwenyewe nipo nipo tu.
Baada ya kama wiki hivi, mara paap kabinti kamekuja kazini kumcheki kaka ake.
Mmh bhas nikafanya juu chini mwishowe nikajikuta naongea nako halafu kakanipa na namba.
Bhasii mambo yakaanzia hapo sasaaa...mapenz moto moto, yani nilikua na muda sijaskia hivyo aiseee.
Bhasi nikagundua kumbe hakana kazi na kanaishi na shangazi yake. Shangazi yake ni nurse so mara nyingi yupo job...mara shift ya usiku mara mchana. So kanashinda peke yake home.
Mwezi wa kumi na moja nikapata safarii huko vijijini kikazi...mtandao ulikua hata haushiki na ukishika ni kwa shida kweli kwelii. Kama wiki moja hivi nikawa sipo sana online.
Ila kabla ya hapo nikamuaga na kumuhaidi zawadi tele teleee
Ile nimerejea kama siku mbili tatu hivi, kakaja gheto kuchukua zawadi zake
So mapenz yetu yakaendelea taratibuuu
Mwezi wa kumi na mbili nikapata tena safarii vijiji vingine hukoo mitandao mibovu vile vile ambapo nilikaa kama wiki.
Dahh sasa awamu hii nimerudi naona mwenzangu kabadilika...nikamuita gheto eti hajiskii vizurii duhh
Nikimpigia simu eti inaitaa tu na message nazo hajibu.
Nikajua hapa kuna kitu tu.
Mara nikapokea sms kutoka namba mpya...eti usimtafute fulani(yani cowards hawa). Mhh na mim mwanaume nikadinda nikampigia akawa hapokei simu...aahh nikaachana nayo.
Sasa juzi kati hapo nimeamka asubuhii nikampigia simu yule mdada...eti kananiambia kana shidah duhhh.
Nikakomaa nae yaniii mpaka nikachelewa kazini siku hio.
Mwishowe kananiambia eti kamepata mimba...halafu kakaongezea etii hawezi kua na mimi tena.
Daahh moyo ulipasuka kidogo ila baadae nikatulia, nikaamka zangu kwenda mishe zangu.
Yanii mapenzii jamanii nishayafungia break...na ndio kwanza mwaka unaanza huo
Ndo hivyo tu wadau...
Sharing is caring jamaniii....
 
Pole sana dogo, mbona ni mambo madogo sana na ya kawaida kwenye mahusiano! Km hakutaki wewe endelea na maisha yako baaade atatokea mwengine mtaanza upya.
 
Kubali yakusumbue sasa baadae utayazoea tu! Hata kama utafumania utaona kawaida tu! Ila yasipokusumbua sasa baadae itakuwa shida sana mimi yalinisumbua enzi hizo ila sasa hata akisema tuachane hata sigeuki nyuma kesho nakuwa na mwingine nae akizingua wala sina haya ya kulumbana nae nasonga mbele kubali yakutese sasa ili yakukomaze kifikira.
 
Tatizo mlango ulioingilia.

Kwenye mahusiano kuna milango mitatu ya kuingilia - au ya kuanzisha - mahusiano;

1. Ngono - mlango huu ukiingilia ni hatari kwa aidha kunogewa na kushahau kuangalia compatibility nyingine ama kutumika na wengine maana mlango huu unafananishwa na elevator. As long as yupo hai, uwepo usiwepo, utatamani kutumika!

2. Sheria - Walau siku hizi mlango huu hautumiki kuanzisha mahusiano. Zamani za wazazi wetu (labda na kwa wahindi bado) ilikuwa mnatafutiwa na wazazi mnakuja kufahamiana siku ya ndoa. Mlango huu pia, pamoja na kwamba ni muhimu lakini si stahiki kuingilia kuanza mahusiano.

3. Pendo/Upendo - Mlango huu ukitumika mara nyingi huwa na mwisho mwema na hata ikitokea bahati mbaya ukafungwa basi maumivu/majuto yake ni tofauti.

Chagua mlango wa tatu maana huo huwa hauna sharing. Waswahili wanasema 'love is like energy, it can not be created nor destroyed, but moved from one person to another.' Mlango huu unaruhusu mtu mmoja tu kwa wakati.
 
Hamia Haloteli mkuu, hutapata matatzo ya kimtandao kabsa adi huko vijijini ndani ndani huko
 
Long weekend Bila kwichikwichi, bia na nyama choma it will be very boring
 
Tatizo mlango ulioingilia.

Kwenye mahusiano kuna milango mitatu ya kuingilia - au ya kuanzisha - mahusiano;

1. Ngono - mlango huu ukiingilia ni hatari kwa aidha kunogewa na kushahau kuangalia compatibility nyingine ama kutumika na wengine maana mlango huu unafananishwa na elevator. As long as yupo hai, uwepo usiwepo, utatamani kutumika!

2. Sheria - Walau siku hizi mlango huu hautumiki kuanzisha mahusiano. Zamani za wazazi wetu (labda na kwa wahindi bado) ilikuwa mnatafutiwa na wazazi mnakuja kufahamiana siku ya ndoa. Mlango huu pia, pamoja na kwamba ni muhimu lakini si stahiki kuingilia kuanza mahusiano.

3. Pendo/Upendo - Mlango huu ukitumika mara nyingi huwa na mwisho mwema na hata ikitokea bahati mbaya ukafungwa basi maumivu/majuto yake ni tofauti.

Chagua mlango wa tatu maana huo huwa hauna sharing. Waswahili wanasema 'love is like energy, it can not be created nor destroyed, but moved from one person to another.' Mlango huu unaruhusu mtu mmoja tu kwa wakati.
Asante sana mkuu
Nimekuelewa sana
 
Back
Top Bottom