Mmemuona Babalevo tu King Msukuma hapana?

Mmemuona Babalevo tu King Msukuma hapana?

HAKI KWA WOTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2022
Posts
2,691
Reaction score
2,303
"....Wabunge 16 ambao tovuti ya Bunge imethibitisha rasmi kwamba wewahi kuingia bungeni wakiwa na kiwango cha elimu ya msingi ni Mbunge wa Geita (CCM), Joseph Kasheku (Msukuma) ambaye ameandika alipata elimu yake hiyo katika Shule ya Msingi Fulwe, Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM), Stephen Ngonyani (Profesa Maji Marefu) aliyesoma katika Shule ya Msingi Kwamndolwa na mwenzake wa Korogwe Mjini, Mary Chatanda.

Wabunge wengine ambao tovuti ya Bunge imeonyesha kwamba wana elimu ya msingi ni Mbunge wa Rungwe (CCM), Saul Amon (S.H Amon), Aziz Abood, Suzane Kiwanga, Mbunge wa Makambako (CCM), Deo Sanga (Jah People), Mbunge wa Kahama Mjini (CCM), Jumanne Kishimba, Mbunge wa Chaani, Khamis Yahya Machano, Mbunge wa Makunduchi (CCM), Haji Ameir Haji na Mbunge wa Paje (CCM), Jaffar Sanya Jussa.

Wengine ni Mbunge wa Tunduma (Chadema), Frank Mwakajoka, Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Mwantumu Dau, Mbunge wa Kilwa Kusini (CUF), Selemani Bungara (Bwege), Mbunge wa Nyang’wale (CCM), Hussein Nassor Amar na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mbaraka Bawaziri"

Hawa wote wamewahi kuwa wabunge wa bunge la Tanzania wenye elimu ya msingi je wote hawakuwa na akili waliowachagua?
 
Back
Top Bottom