Mbugi
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,488
- 257
anakwazwa na LI MFUMO otherwise ni rais jasiri
mfumo (kwamaana ya taratibu/kanuni za kiutendaji, sheria zetu hasa hizi zilizoasisiwa na mafisadi kwa maslahi yao, na swala la kila mtu asikilizwe yaani haki za binadamu kwa maana ya hata hao waliotufikisha hapa nao walindwe kwa madai ya haki pamoja na ufisadi walioutenda, mfumo unaomjali sana mkubwa/kiongozi kwa kumpa posho kubwa kubwa, kama sheria ya mafao kwa viongozi wa kisiasa ya mwaka 1999, unaweza kuona namna ambavyo imelenga kumpa mapato makubwa huku ikimchilia mbali mtumishi yeyote kama mwal aliyefanya kazi kwa zaidi ya miaka 36 kwa kupata 36m/= huku mbunge/mkuu wa wilaya nk akipata 92m/= mpaka 130m/= kwa madai ya kumpatia winding up allowance ya 50% ya mshahara wake kwa miaka 5 na 50% gratuity. kwa ujumla mfumo uliopo unahitaji kwanza wakuu wetu kwanza kujikana nafsi zao, warudi kwa watu kwa kubadili sheria/mfumo uliopo.