Mmarekani huyu amenishangaza.

Mmarekani huyu amenishangaza.

Pastor Achachanda

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2012
Posts
3,023
Reaction score
1,316
Wakuu,bora kuuliza kuliko kujifanya unajua.
Leo katika pitapita zangu nimekutana na mmarekani ambaye ameniacha kwenye mataa.
Nilisogea karibu na gari lake akiwa na mkewe wameketi jirani na gari. Sasa simu ndani ya gari iliita akataka afungue mlango akaichukue lakini mkewe akamwambia kuwa atumie rimoti na wireless headphone kupokea simu. Akasema kuwa alisahau ngoja afanye hivyo. Nikakuta amepokea kwa rimoti akaanza kuongea. Nikatamani nione hadi hatua ya mwisho. Kisha akatumia rimoti kumaliza maongezi. Nikabaki nashangaa,nimetoa macho kama mjusi aliyebanwa na mlango.
Sasa naomba kuuliza, je, simu kama hizi hapa Tanzania zipo?Bei zake zikoje?
Asanteni. Nawasilisha.
 
Mkuu.Imezoeleka siku hizi. Hawakawii kukuambia:"Weka picha".
 
Hyo ni kawaida tuuu, unaweza kutumia earphones zako ambazo ni wireless kupokea simu..Ila inabid usiwe mbali na simu yako coz network coverage yake ni ndogo..
 
halafu sio kila unapoona me na ke wako pamoja ukadhani ni mke na mume,unaweza kukuta wanatoka chama kimoja huko walikotoka wametoroka safari za kibunge
 
Wakuu,bora kuuliza kuliko kujifanya unajua.
Leo katika pitapita zangu nimekutana na mmarekani ambaye ameniacha kwenye mataa.
Nilisogea karibu na gari lake akiwa na mkewe wameketi jirani na gari. Sasa simu ndani ya gari iliita akataka afungue mlango akaichukue lakini mkewe akamwambia kuwa atumie rimoti na wireless headphone kupokea simu. Akasema kuwa alisahau ngoja afanye hivyo. Nikakuta amepokea kwa rimoti akaanza kuongea. Nikatamani nione hadi hatua ya mwisho. Kisha akatumia rimoti kumaliza maongezi. Nikabaki nashangaa,nimetoa macho kama mjusi aliyebanwa na mlango.
Sasa naomba kuuliza, je, simu kama hizi hapa Tanzania zipo?Bei zake zikoje?
Asanteni. Nawasilisha.

Smart phone, Bluetooth na internet access mkuu....
 
Pole ndugu yangu yangu kuuliza ni kuongeza ujuzi. Simu yeyote yenye bluetooth inaweza kutumia wireless. Umbali kutoka kwenye simu hadi kenye bluetooth unategemea ubora wa bluetooth. Kuna bluetooth za kuzungumzia tu na kuna zingine za kuzungumzia na kusikilizia mziki.(si radio) ila hayo matumizi yanatumia betry kwa wingi kwani zote ni za kuchaji.
 
halafu sio kila unapoona me na ke wako pamoja ukadhani ni mke na mume,unaweza kukuta wanatoka chama kimoja huko walikotoka wametoroka safari za kibunge

hehe, wako kidubai dubai sio?
 
hehe, wako kidubai dubai sio?

hahahahaaa, wakikusikia!afu hata hawakanushi, kudhihirisha ni kweli, wanaita 'character assassination', wana tu-terminology twingi kweli
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom