Mliwashirikisha wananchi kuhusu Tozo kabla ya kuwakata?

Prof Koboko

JF-Expert Member
Aug 15, 2020
350
2,549
Tumefikia hatua ambayo serikali unalazimishwa wananchi kufanya itakacho, yaani mnaandaa mswada wa sheria kimya kimya kisha mnaupeleka bungeni kwakua mnajua udhaifu wa lile bunge inapitishwa mkaanza kuwalima Tozo wananchi bila ridhaa yao, huu ni uonevu uliokubuhu. Wananchi sasa hawana maamuzi kuhusu hata rasilimali zao binafsi.

Wadau wa mitandao ya simu wanalia kua hawakushirikishwa sawa sawa kisha mkafanya maamuzi yenu, hii si sawa. Taifa gani ambalo raia hawana maamuzi? Hatima ya mambo haya itapatikana tu siku wakichoma.

Kwa kuonesha kua wananchi hawakuashirikishwa kabisa pale kelele zilipozidi Mhe Rais akaamuru tozo hizo zipunguzwe, cha kushangaza Mwigulu Nchemba alikomaa mpaka mwisho kua asiyetaka tozo ahamie Burundi. Maana Mwigulu angekua ndio Rais wa nchi wananchi wangelimia meno. Kingozi anayependa sifa, majivuno na kiburi aina ya waziri huyu watalipeleka taifa pabaya sana.

Tozo za Majengo zimechomekwa ghafla kwenye LUKU bila kuwashirikisha wanançhi matokeo yake sasa ni vilio kila mahali mzigo imeangukia wapangaji, eti mkadai pesa zenu kwa wamiliki wa majengo, yaani mpangaji akadai pesa yake kwa mwenye nyumba? Kwa utaratibu upi mliowawekea?

Hakuna anayekataa maendeleo katika taifa lake, mbinu mliyoitumia kukata pesa za watu ni haramu si shirikishi, tunaokatwa hatukubaliani na utaratibu huo hata kama ingekua tunakatwa senti moja.
 
Ilisemwa mahali kwamba wananchi wamekubali tozo, madelu kama stelingi wa tozo......alianza na bil. 48, baada ya muda mfupi akaja sijui na bil. 96 na takwimu za vituo 255 vya afya, madarasa 500 blah blah....and blah blah....ili ajaribu kuwa impress wananchi. Mimi mwanakijiji wa hapa kazilankanda sijui hivyo vituo 255 vinavyosemwa vimejengwa wapi!? na hayo mabilioni yaliyokusanywa yamehifadhiwa wapi!? nipo hapa navizia vizia kama kuna tetesi zozote za mgao wa pesa ya mboga msisite kunistua...
 
Hizi bla blah eti vituo 250, vimejengwa wapi? na nani? kwa utaratibu upi? Mtaalamu mshauri ni nani? Mkandasi ujenzi ni nani?
Watumishi w afya watatoka wapi?

Je bajeti iliacommodate? Hizo blah blah zao
 
Back
Top Bottom