Mlipuko watokea katika kiwanda cha kusafisha mafuta mashariki mwa Saudi Arabia

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,992
17,892
Mlipuko watokeo katika kiwanda cha kusafisha mafuta mashariki mwa Saudia

Shirika la Kitaifa la Mafuta nchini Saudi Arabia ARAMCO limetangaza kutokea mripuko katika kituo cha kusafisha mafuta, mashariki mwa nchi hiyo.

Taarifa iliyotolewa na shirika hilo imesema kuwa, kwa akali watu wawili ambao ni wafanyakazi wa kituo hicho cha kusafisha mafuta wamefariki dunia. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mripuko huo umetokea katika kituo cha Al Jubail kilichopo mkoa wa Mashariki nchini humo.

Hii ni katika hali ambayo baadhi ya vyombo vya habari vimetangaza kuwa watu 18 wameuawa na kujeruhiwa katika tukio hilo. Hata hivyo shirika hilo la kitaifa la mafuta halijatoa taarifa zaidi juu ya chanzo cha mlipuko huo kwenye kituo hicho.

Itakumbukwa kuwa baada ya wanamapambano wa Yemen kushambulia na kuteketeza taasisi za mafuta za Saudi Arabia mwezi uliopita, dhirika la ARAMCO lilikumbwa na mgogoro mkubwa wa fueli kiasi cha kulazimika kununua nishati hiyo kutoka India ambayo nayo inanunua mafuta kutoka Iran

My take: Naona kimeanza kunuka Iran vs Saudia.

Chanzo: ParsToday
 
4bsle31a5cbe6a1i59i_800C450.jpeg
 
... naona Ayatollah anacheza na moto! Atapotezwa jumla na utawala wa kidini chini ya cheo kijulikanacho kama Ayatollah utapotea mazima; utasomwa kwenye makaratasi na watoto huko mashuleni kwamba Iran iliwahi kuwa utawala wa aina hii!
 
"E="Mazindu Msambule, post: 33167302, member: 71865"]
HUaga sielewi labda nieleweshwe; hivi unapo sema "hi ndio imebaki kua faraja yenu" hua unamaanisha nini? Iran na Saudia wote ni Waarabu na wote ni waislamu sasa kwa huku bongo inakuaje mtu anachagua upande wakati wote hao hawatuhusu?
[/QUOTE]
Ukiona hayakuhusu wewe sio lazima yawe hayanihusu mimi!
 
... naona Ayatollah anacheza na moto! Atapotezwa jumla na utawala wa kidini chini ya cheo kijulikanacho kama Ayatollah utapotea mazima; utasomwa kwenye makaratasi na watoto huko mashuleni kwamba Iran iliwahi kuwa utawala wa aina hii!
Umenichekesha sana kwa hizo ndoto zako za abunuwasi
 
... naona Ayatollah anacheza na moto! Atapotezwa jumla na utawala wa kidini chini ya cheo kijulikanacho kama Ayatollah utapotea mazima; utasomwa kwenye makaratasi na watoto huko mashuleni kwamba Iran iliwahi kuwa utawala wa aina hii!
Endeleni kujifariji mkimaliza mkalale mukue wakubwa
 
HUaga sielewi labda nieleweshwe; hivi unapo sema "hi ndio imebaki kua faraja yenu" hua unamaanisha nini? Iran na Saudia wote ni Waarabu na wote ni waislamu sasa kwa huku bongo inakuaje mtu anachagua upande wakati wote hao hawatuhusu?
IRAN ni Waislam Ila Sio Waarabu Halaf Hakuna anaechagua upande ila kuna wanao simamia hakki mfano IRAN Ss hv ageuke awe na tabia za SAUDIA na SAUDIA Awe na Tabia Za IRAN Tutaenda Msapoti MSAUDIA
 
Mmoja Mshia,mwingine Msunni

Back
Top Bottom