Tatizo wala sio Malaria ya watu,tatizo kubwa ni UKIMWI.Unajua Dar watu wengi wanaumwa ila hawaelewi kwanini Vipimo vya Ukimwi vinasoma Negative wakati wao kwa jinsi wanavyoumwa wanajijua kabisa hawawezi kukosa UKIMWI na wanagongana sana wasife wenyewe,Nadhani Wizara ya Afya iangalie upya Vipimo vya Ukimwi kama viko sawa basi kuna Ugonjwa Mwingine unaofanana na UKIMWI umeingia,wasipokazana hapo wataisingizia sana Malaria ya watu.
Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
Kwa hiyo ukiupata dengue ni kifo tu?
Sio DENGE, Bali ni Dengue fever or Dengue Haemorrhagic fever
Huu ugonjwa kiboko.samahani ivi dengue inatamkwaje? Maana wengine watamka DENGU, DENGI DENGE napata tabu sana
Very well said. Halafu sijajua kama kama wanatumia recommended dose au bado wanatumia SP?
Inatamkwa DENGU mkuu
ni kweli tatizo la malaria ni dar nzima...mabadiliko ya halu ya hewa na sijui labda ni wale mbuu waliyokuwa kwenye madimbwi kule muhimbili...ila malaria imewapata asilimiaa kubwaaa na hadi kuua imeua..naona serikali kupitia wizara ya afya wako kimyaa...hawaja chukua hatua yoyote mpaka sasa
Niugua from tar 23 march nilikutwa na Malaria 3 nikatumia mseto hakuna nafuu, nikaenda kwa Dr. Mvungi ikakutwa imeongezeka hadi imekuwa malaria 6 nikalazwa 3 days nimetundikiwa Quinine nilivyoruhusiwa nikapewa duo-cotexin nikazimaliza! Ikapungua ila haikwisha nikarudi tena hapo kwa Dr. Mvungi nikaambiwa bado ipo Malaria 2 nikapewa Quinine ya vidonge nikameza siku ya kwanza ya pili nikaenda kumsalimia mtu msasani nikajisikia kukaukiwa sana yaani mate yanakauka kabisa mdomoni nikawahi TMJ nikatundikiwa Drip mbili za maji nikachukuliwa damu kwa further checkup Nikaambiwa nistop zile dawa za QUININE from that Moment!
Baadae majibu yakaja nikakutwa kwingine(liver function, kidney function e.t.c) kupo Ok ila nikaambiwa inaonyesha kwenye blood kuna infection(Maybe ndo hiyo Malaria) nikapewa dawa fulani hivi kwa siku 5 nilivyorudi nikapimwa nikaambiwa Malaria hakuna tena! Nikaenda sehemu nyingine wakaniambia tena hakuna Malaria!
Nimeumwa almost 3 weeks!
Ila namshukuru Mungu sasa hivi niko very ok!
RockSpider tupia jicho uzi huu.sasa hivi dar kuna mlipoko wa DENGUE FEVER.dalili zake zinafanana sana na maralia.ushauri wangu.ukipata homa kali(namaanisha mwili kupanda kwa joto lake)nenda mwananyamala hosp.pale kuna kituo kinaitwa FEVER STUDY wanapita vipimo vingi kikiwemo na hicho cha DENGUE FEVER.pale itajulikana kama ni malaria au dengue.mshauri hili na mwezio.
hapana.sio ndo kifo.ni selflimiting.inaisha yenyewe ndani ya siku kumi au zaidi.kinachotakiwa ni kushusha homa n.ingawa mara nyingine yaweza kusababisha kutokwa na damu puani na maeneo mengine mwilini.
Nimemaliza metakeflin ,nimepima leo wamesema wapo waili.
Nimegonga mwarobaini jioni nasikilizia,asubuh nishtue tena.