FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 40,859
- 46,977
Ni jambo lililonishtua hasa kwa maeneo ya Tabata.., kila nyumba ninayoingia hukosi mtu anaumwa malaria.., tena utaambiwa kuna wengine wawili watatu nyumba hio hio wamepona juzi juzi tu.., kibaya utaambiwa wameshamaliza dozi ila hawajapona kwa hiyo wanaendelea na sindano.., jamani kwengine vipi huko..?
Sasa ni kipindi cha mvua nyingi madimbwi yamekuwa mengi tujitaidi usafi wa majumbani pia hayo madimbwi yasiyokauka kwa sasa ndio hatari yanazalisha mbu kwa wingi sana na magonjwa mengine kama vichocho tuwe makini na watoto wanapocheza, lakini tukisema kila jambo hata yale ya tahadhari tuiachie wizara ya afya itakula kwetu .
Ni jambo lililonishtua hasa kwa maeneo ya Tabata.., kila nyumba ninayoingia hukosi mtu anaumwa malaria.., tena utaambiwa kuna wengine wawili watatu nyumba hio hio wamepona juzi juzi tu.., kibaya utaambiwa wameshamaliza dozi ila hawajapona kwa hiyo wanaendelea na sindano.., jamani kwengine vipi huko..?
huo ni ugonjwa unaitwa DENGE dalili zake na km za malaria na hauna tiba zaidi ya kunywa maji mengi
Malaria inaongoza kwa vifo kuliko ugonjwa mwingine kwa sasa Tanzania, ndiyo maana tunabadilishana neti na madini,..
Viva CCm
Mis-diagnosis. Pitia maabara kabla hujasema malaria