Mlipuko wa bomu wauwa watu 3 nchini Colombia

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,604
2,000
Wanawake watatu wameuwawa, katika kile wakuu nchini Colombia wanasema kuwa, shambulio la kigaidi katika mji mkuu Bogota.

Mlipuko huo ulitokea katika soko moja la biashara la Zona Rosa, katika mji mkuu Bogota.
Watu wengine 11 wamejeruhiwa katika shambulio hilo.
Meya wa Bogota, Enrique Penalosa, amesema kuwa mmoja wa wanawake aliyefariki anatoka Ufaransa.

Wakuu wanaamini kuwa mlipuko huo ulitokea ndani ya choo cha wanawake, baada ya bomu dogo kulipuka.

Mlipuko huo ulitokea Jumamosi alasiri wakati wa shughuli nyingi, katika soko hilo la kibiashara, pale lilikuwa limejaa wateja, waliokuwa wakinunua bidhaa za siku kuu ya kina baba Duniani-- ambayo inasherehekewa leo siku ya Jumapili, Juni 18.

Haijabainika ni nani au kundi lipi, lilitekeleza shambulizi hilo.


BBC Swahili
 

Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
7,215
2,000
Makundi ya kigaidi kila mahali duniani.Lini dunia itakuwa sehemu salama??!!
 
Apr 4, 2017
84
125
Makundi ya kigaidi kila mahali duniani.Lini dunia itakuwa sehemu salama??!!
Wewe kwanini utaki kujirekebisha umekua mropokaji marakwamara waliofanyiwa tukio hawajabaini ninani aliyefanya hivyo. Kwauchunguzi gani uliyoufanya mpaka unathibitisha hao waliofanya hivyo nimagaidi???
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom