Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 8,274
- 25,322
Sasa watafiti wa macho wamekuja na tathmini yao kwamba, kadri siku zinavyosonga mbele katika miongo minne ijayo, idadi itakuwa mara tatu ya ilivyo sasa.
Asasi ya afya iitwayo Lancet Global Health, inasema makadirio yaliyopo ni kwamba, watu wenye matatizo hayo ya kuona wanaongezeka kutoka milioni 36 wa sasa, hadi milioni 115, ifikapo mwaka 2050. Ni ongezeko la asilimia 319.
Namna ya kukabiliana na hilo, wasomi watafiti hao wanashauri kuwapo uwezeshaji wa kutosha katika eneo hilo la tiba ya macho. Hiyo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa katika jumla ya nchi 118.
Macho yanayotajwa kuwa na kiasi kikubwa cha wagonjwa ni katika maeneo ya Bara la Asia na Kusini mwa Jangwa la Sahara, barani Afrika.
"Hata kama kuna tatizo dogo la uono, linaweza kuwa tatizo katika maisha ya mtu," anasema, mtaaluma Profesa Rupert Bourne, kutoka Chuo Kikuu cha Anglia Ruskin.
Anaongeza:”Kwa mfano inapunguza uhuru wao kwani wakati wote wanakwazwa. Inamaanisha, watu wanazuiwa kuendesha."
Chanzo: BBC