Mlipuko mkubwa watokea kwenye Kanisa Katoliki Arusha, watu kadhaa wajeruhiwa

Status
Not open for further replies.
Lema: hili tukio limetusikitisha sana. Ni moja ya matukio ambayo tumeyasemea huko nyuma, kwamba vyama vya siasa baada ya kukosa umaarufu waliamua kugawa watu kwa siasa za udini. Haya ni matunda ya siasa chafu za kidini zinazoendelea kuenezwa na ccm na serikali yake. Redio maria wamekata matangazo ya moja kwa moja.
hapa kuna umuhimu wa kuanzisha media yetu tuwe tunapata makavu live
 
radio maria why mmemkata lema
wacha tunmsikilize maoni yake.
wala hamwezi kuwa liable kwa kauli yake kama chombo cha habari
tusubir bungeni kesho sijui itakuwaje
 
Lema anasema:

- Ni tukio la kushtua.

- Vyama vya siasa vimetumia kete ya udini.

- Hakuna jambazi anaweza kutupa bomu kanisani.

- Police watatumia nguvu nyingi kama walivyotumia kunikamata mimi.
 
Lema alikuwa anaongea ghafla redio imekata na kuanza kuimba nyimbo,lakini alikuwa amesha sema kidogo kuhusu muendelezo wa siasa za ukanda za ukabila na udini zilizoasisiwa na vyama vya siasa vilivyoanza kupoteza umaarufu,wakuu mlioko Arusha mtufamishe wamemkamata tena lema au ni redio tu imekatisha?
 
Hapa Lema kaharibu tena. Naona Radio Maria wameamua kumkatisha. Huyu Lema naye wakati mwingine ni kichwa maji sana. Yaani kwenye tukio kama hili analeta hoja za UCCM? Anataka kuwapandisha hasira waliopo hapo kwenye tukio au anataka nini? Ni kweli watu tunampenda Lema ila kusema ukweli wakati mwingine uwezo wake wa kuchambua mambo ni ziro kabisa.
 
Hivi Lema anatafuta sifa ili iweje?
Mimi naanza kuwa na wasi wasi na akili ya huyu bwana.
Masuala kama haya inabidi mtu uchunge kauli yako na sio kuweka petroli kwenye moto
Kukamatwa kwake na bomu la leo kunahusiana n nini?
 
Mungu awaponye majeruhi, Ee mwenyezi Mungu huhitaji kupiganiwa ili ujidhihirishe, tunakuomba utuepushe na ushetani huu Amina.

Kweli Mungu hapiganiwi! Lakini iko haja ya self-defence mechanism.

Tutapigwa sana mpaka tutazinduka toka usingizini.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Naona Lema alikua anamwaga sumu redio Maria wamekatiza matangazo.
Alishaanza kutema simu kuhusu kuhusu ccm.
 
Wakuu ghafla Mbunge wa Arusha akiongea ametoweka hewani na sasa nyimbo zinapigwa nani mwenye taarifa za tukio hili toka eneno la tukio?Wameogopa maoni yake?
 
hiyo tumeinasa hiyo.....wamemkatia kamanda lakini ujumbe umefika......
 
Kisa vitu alivyo kuwa anazungumza Lema...ya kwamba anaamini polisi watatumia nguvu ya kuwasaka watuhumiwa kama walivyo mvamia nyumbani kwake usiku....pia anasema ya kwamba wafanya hilo tukio si majambazi kama ni visasi vya kijambazi wata hufatywa majumbani au madukani nk nasi kanisani amechana live yakwamba CCM ndiyo ilipanda hizo siasa za kidini na ukanda na hayo ndio matokeo yake...navumilia tuu navumilia tuuu nalia kwa uchungu machozi yanatililikaaaa NAVUMULIATUUUUU maaana nateseka....wimbo waendelea
 
Mulongo Kapata Fundisho, Leo Kaanza na Kuto Pole
Nilifikiri ataleta Dharau, ila Ngoja nendelee Kumsikiliza, haaminiki Kabisa Huyu

hivi mulongo amesaidia kufanya uhokozi au ameangalia tuu. poleni sana wana ARUSHA
 
Hili tukio linanikumbusha ule msikiti pembeni mwa soko la Kilombero maarufu kwa mafunzo ya ugaidi. :behindsofa:
 
M23 wameanza Kazi kwa vitendo siye tumekalia maneno tu........!
Haya Mh. Membe yupo wapi sasa......!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom