Hongera sana kaka kwa nafasi adhimu uliyoipata,kambi ipo nje kidogo ya mkoa wa kigoma katika ufukwe wa ziwa Tanganyika na ndio kikosi senior miongoni mwa vikosi vya j.k.t nchini.Mafunzo sio magumu sana to the extent that hayawezi kufanyika.Vitu viwili vya msingi vya kuzingatia ni uvumilivu na morali.Ukumbuke kazi ya kumbadili RAIA kuwa ASKARI sio lelemama,so utapigwa mzigo wa maana,kero nyingi na maovyoovyo ya kutosha ili uwe askari kweli.Mengine mengi utayajua huko huko na believe me ukiwa mvumilivu na una morali utadumu chomboni.Kama alivyosema mdau hapo,sitegemei pia utoroke maana hakuna sababu ya kufanya hivyo.Najua mmeshaambiwa kwenda na trunk(soldier box),nguo chache za kiraia(usiende na nyeupe,kuna udongo mwekundu Kigoma),napendekeza tracksuit nyepesi,uende na viatu vigumu vya ngozi maana zile sare zao huwa zinachelewa sometimes.Uende na dawa baadhi za magonjwa madogo madogo ambayo huwa yanakusumbua mara kwa mara koz kule unatibiwa kijeshi pia.Mahitaji madogo madogo kama dawa ya meno,mafuta ya mgando(haya ni muhimu sana kutibia fangasi na kuapply kwenye nyayo),mswaki,nguo za ndani,nyembe za kunyolea para na usisahau fedha maana huwa kuna dharura zinatokea na simu huwa zinakusanywa.Kwa sasa niishie hapa ila kwa mwenye swali atauliza hapa