Usajili wa chuo cha ufundi ni kiasi gani cha fedha?

Gutapaka

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
283
218
Natumaini mu wazima wa Afya. Poleni Sana wenzangu walio dhaifu kiafya.

Naomba Mnitoe tongotongo wadau wangu. Kwa Muda mrefu nimekuwa nikifuatilia Usajili wa Chuo cha Ufundi. Lengo langu lilikuwa ni Kutaka kujua gharama za Usajili kwa mchakato mzima.

Zaidi ya yote, nikipiga simu Nacte hawapokei na VETA vivo hivyo. Kwa hiyo mpaka leo sijafanikiwa kujua chochote. Niliwahi kumuuliza mkufunzi mkuu wa chuo Fulani cha VETA akaniambia VETA wao hawahusiki kwa sasa bali NACTVET.

Tafadhali, naomba kwa anayefahamu anisaidie mchakato mzima wa Usajili unaweza gharimu kiasi gani na ipi ni njia sahihi ya kufanikisha mchako huu.

NAOMBA KUWASILISHA.
 
Cheki website ya nacte kama ina taarifa au Google. Institutions zetu shida sana simu zao kama urembo tu. Kama uko dar basi watembelee.
 
Mkuu kipindi VETA ipo yenyewe gharama ilikua ni 50,000 Tshs kwa sasa hivi imeenda NACTVET sijui ni kiasi gani ila kipindi cha nyuma NACTE wao gharama ilikua 5m hapo hakuna guarantee kama utafanikiwa au laa..kwaio cha msingi kama upo Dar nenda kule NACTVET ni karibu na chuo cha kodi wakakupe muongozo pia sifahamu kama NACTE wana matawi mikoani maana hujasema upo wapi...
 
Back
Top Bottom