Kilaza Flani
Member
- Oct 27, 2011
- 61
- 2
- Thread starter
-
- #61
Inawezekana tunakushauri tuu hapa ila kumbe huna mpango wala effort zozote za kumtafuta huyo mke.
Umefanya juhudi gani kutafuta mke
Umejiwekea lengo gani na kwa muda gani kumpata huyo mke
Na je vigezo gani umeweka kumpata huyo mke
Na je unatafuta mke wa kuoa mwaka huu au mwakani au baada ya miaka mingapi
Kwanza jiulize ulishajitambua ni mwanamke wa aina gani unamtaka,
Coz kuna baadhi ya wavulana japo wanakuwa wanona ni wanaume ukimuliza aina ya mke anayetaka hizo sifa anazotaja mpaka aibu kwa uankuta kabase kwenye sifa za nje ambazo ni ngumu kwa mtu mmoja kuwa nazo zote labda mpaka kutoa oda kwa mungu amtengenezee,so kumpata inakuwa ishu,
Nakushauri tuliza akili,mke sio sura wala umbo,mshirikishe mungu ktk kumtafuta utampata tu coz kila mtu kaumbiwa mtu wake,
Jiweke km mwanaume alietayari kuwa baba wa familia sio ujiweke kivulana utaishia kupata visichana mcharuko,
Hata ukimpata anayefanania kuwa mke uwe na subira na mvumilivu kwan wengi huwa hawakurupuki kukukubali ni lzm auone userious wako,pia angalia namna unavowaaprochi,ulimi wako ndio silaha pekee hata km utakuwa na mwonekano wa aina gani!
Epuka kutumie pesa km ushawishi wakati wa kujieleza ni sumu kali kwa wadada walio makin,japo wengi hawaamin hili.
Ikifika siku Mungu atatuma malaika uitaona anakuonyesha huyu ndo mke wako.
Lakini wewe hutamuona malaika.
Songíto;3208307 said:kaka shukuru unapata kugundua kuwa wenzio unaokuwa nao sio waaminifu!! kuna watu hawakugundua hayo mapema, au waligundua ila wakalazimisha kuingia kwenye ndoa, wakazaa na kuanza maisha kwenye ndoa zao, saizi wanaonja shubiri (chungu) kwa maisha magumu ya ndoa... naomba nikutie moyo mkuu kuwa "mke bora hutoka kwa bwana (muumba)". Ukiona hivyo ujue bado muumba hajakutengea wako!!!
ILA...ILA.... kama nawe umekuwa ukiwatendea wenziwako ndivyo sivyo, inawezekana muumba anafanya malipizi kwa mabaya hayo uliyotenda maana "Muosha Huoshwa", kama ndivyo, tubu mrudie muumba na omba misamaha kwa wabaya wako na halafu mpigie magoti muumba wako na omba mke bora, atakupa nakuambia...
Mshirikishe Mungu katika hatua hii ya kumtafuta mke wa kuoa maana mke sio nyanya ambazo unaweza kwenda soko lolote na kuchagua nyanya kwa muuzaji yyote unayekutana nae
Mke ni mtu ambaye ni muhimu sana kwako na mtu ambaye ije mvua liwepo jua usiku na mchana sometime mtakuwa wote na mtashare mengi so unatakiwa kuwa makini sana kwenye uchaguzi wako
Sio kweli kwamba wengi ni mcharuko ila may be wewe mwenyewe hujatulia na ndo maana kila unayempata anafanana na wewe
Jipe muda na tulia kwenye safari hii ya kumtafuta mwenza
Kilaza,
Ndugu yangu mke huwa hatafutwi, yani inatokea tu una date mtu hadi unaona mmh hapa sasa sina ujanja.
Mwenzako mimi nilikuwa nimemaliza chuo nipo kitaa sina kazi full kujirusha tuu na washikaji naanza starehe Alhamisi namaliza Jumapili na sitoki club had nisikie swalaaa swalaa lol...kipindi hiko sina hata mpango wa kuoa mtu akisema swala la ndoa namuona mshamba and thats when i met MRS Right.
Nilikuwa na mshikaji tunatoka usiku one akapigiwa simu na cousin yake binti aliyekuwa anasoma chuo Dsm akiomba twende tuka wa pick hostel coz nae alikuwa na shosti wake wangependa kwenda out. Mshikaji alichomoa,lakini nikamsihi tukawachukue after all itakuwa poa kuwa na company. That night nili dance sana na cousin yake mshikaji huku jicho langu lipo kwa shosti wake na cousin. Maana alikuwa anang'aa hadi balaa.Offcoz mshikaji alikuwa ana dance na shosti mtu ambaye ndio my waifu wangu kwa sasa. After hapo tuka date kwa takriban miaka 4 alikuwa akitaja swala la ndoa ananitibua lakini finally nikaoa huyo huyo.
inawezekana anakupa wa kufanana na wewe, badilika uone.
Leo hii ukiniuliza nilimpataje mama Ngina hata sikumbuki...................... haya mambo huwa yanatokea Automatikale.
Nimesoma hizi comments hakika nimeona busara zenu, i hope kwa wale wote wanaosaka ndoa watanufaika na mashauri haya. Kila la kheri waJFIla kweli mkuu wanawake wengi nimcharuko lakini siyo wote wewe jitaidi kutafuta kanisani kwako na pia umuombe mungu
Dah! Sijui nikupe nini mtoto wee mweeeee umeongea point mpaka nimesisimka.
Nimefarijika sana na ushauri wenu.Thanks guys ngoja nami nijipange upya,possibly nilikuwa nakosea.
Tatizo wanaume micharuko pia mnataka waliotulia. Tuliotulia wenyewe tupo wachache. Hebu oeni micharuko yenu hyo hyo.
Huna nia ya kuowa. Wanawake wote waliopo duniani!!!!!! Mbona mimi wananifwata wenyewe niwaowe$$$
kama unawataka wa humu humu badilisha id
Husninyo kweli hututakii mema kuoa mcharuko aise noma
Mwanaume mcharuko anaweza kutulia bana
kama unawataka wa humu humu badilisha id
kwani mwanamke mcharuko hawezi kutulia?
Anaweza na inategemea kampata mwanaume wa aina gani
Ila mcharuko kwa mcharuko ni balaa hapo
tena sio balaa dogo. Ukimpata aliyetulia japo kidunchu unashukuru mungu.
Wewe una gundu.
Jichunguze :tabia/fikra/hobbies/muelekeo wa maisha/unavyojionyesha au onekana, chunguza vigezo unavyotumia kutafuta/chagua mpenzi, chunguza matarajio yako kama yanaendana na eneo unalowinda n.k
Ningekua mwanaume na nimeoa ningekwambia pa kwenda
kabisa
Ila yote ni kumuomba sana Mungu akupe mwongozo wa yule ambaye atakuwa mke bora kwako