Mliooa au Mnaotarajia kuoa Jiandaeni Kisaikolojia

Simplicity.

JF-Expert Member
Dec 19, 2013
2,636
1,656
Kadri muda unavyoenda idadi ya ndoa zinazovunjika inaongezeka.

Matokeo ya research yangu niliyoifanya hivi karibuni yameonyesha kuwa kufikia mwaka 2025 karibu 3/8 ya ndoa zinazoibukia hivi karibuni zitavunjika na takribani 75% ya ndoa zitakazobaki zitakuwa na hali mbaya zaidi za kimahusiano.

Ndoa zinazoongoza/zitakazoongoza kuvunjika ni za wanandoa wenye umri kati ya miaka 25 - 40 lakini wanaopishana umri wa miaka michache, kati ya 1 - 4.

Hata hivyo, matokeo yameonyesha kuwa 80% ya ndoa za sasa zina mikikimiki na misukosuko isiyoisha, na 60% ya ndoa za wanandoa wenye umri zaidi ya miaka 40 ni mfu kwa maana kuwa wanandoa hao hawana kivutio chochote cha kimapenzi na kimahusiano kinachowaweka pamoja, zaidi ya mambo mengine kama vile imani za kidini, watoto, mali, ndugu, majirani, marafiki, n.k., ambavyo wengi wao huwaza mustakabali wake mara watakapoachana.

Mahusiano mengi kwa sasa hasa yenye umri wa kuanzia miaka 5 na kuendelea, hata kama ni magumu kiasi gani, yanashikiliwa na mitazamo ya wahusika na ya jamii kwa sababu ya wahusika kuogopa kutoa taswira mbaya kwa kuachana.

Mambo kadhaa yanayochangia ndoa kuvunjika kwa kasi ni pamoja na umaskini, mwanandoa mmojawapo kutokuwa na uwezo wa kuzaa, michepuko, uchochezi wa ndugu, jamaa, majirani, marafiki, kukuta mambo au mwenzi ni tofauti na matarajio, ujinga - ukosefu wa elimu au kuwa na elimu feki kuhusu mambo ya mahusiano.

Ndoa zinazoongoza kuvunjika zaidi kwa sababu ya michepuko na wivu wa kimapenzi ni zile changa, ndoa zilizodumu kwa miaka 10 na kuendelea huvunjika zaidi kwa sababu tofauti.

Matokeo pia yameonyesha kadiri muda unavyosonga, wanaume wengi wataoa wakiwa na umri mkubwa, kati ya miaka 34 - 45 na kutakuwa na mahusiano mengi zaidi ya kindoa yasiyokuwa rasmi, wakati wadada wenye umri huo wengi wao watakuwa tayari kuolewa kama mke wa pili, tatu, etc., (wengi zaidi ni kwa siri) - small houses, na hii itaongeza suluba kwa wanandoa (wanawake) wakongwe kwa sababu akina dada wa umri huo wateja wao wakubwa ni wazee, wenye umri wa miaka 50+, kwani wadada wengi wa umri huo huogopa sana mikikimikiki na fujo za kimahusiano.

Vile vile kuna ndoa nyingi zinazovunjika kutokana na kukosekana uvumilivu baada ya mzazi mmojawapo kugundua au kuhisi amesingiziwa mtoto.

Utafiti pia umeonyesha kuwa, kuna kasi tofauti za uvunjikaji wa ndoa kulingana na nature ya compositions za wanandoa kama vile, kazi wanayofanya, kiwango cha elimu na miingiliano mingine ya kijamii.

Ni wakati mwafaka sasa kwa wanandoa au watu wanaofikiria kuoa kujiandaa kisaikolojia ili kupunguza athari pale mahusiano yao yatakapoingia mushkeli au kuvunjika.

Hakuna dawa wala dalili yoyote ya kupatikana kwa suluhisho la matatizo ya kimapenzi, kwa sababu katika mahusiano kila mtu ni dereva na ameshikilia usukani muda wowote hivyo anaweza kuzembea au kuamua kwa makusudi kuendesha gari vibaya na kusababisha ajali.

Matatizo ya ndoa ni general trend with time na dawa yake ni ngumu kupatikana kuliko ya ngoma.

NB: Kuna exceptional few (the chosen, perfect couples) tunaosail ndani ya ndoa smoothly.
 
Aaah kuoa nitaoa na ndoa yangu itadumu kwa raha mustarehe,labda we jiandae kwa hayo.
 
Usizunguke na maneno mengi, michepuko ni laana

Hili tatizo linashika kasi kila siku
 
Mi Sina plan ya kuoa/ nimeona huu utafiti ndo najiridhisha kabisa...ni stress tu ..
 
LifeHacker wewe yako ina nini unachoita perfect, exceptional or chosen na ina miaka mingapi???!!!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom