1. Barabara za lami nyingi kuliko za awamu zote za kabla yake ukichanganya pamoja.
2. Shule za Sekondari nyingi kuliko za awamu zote za kabla yake ukichanganya pamoja.
3. Wanafunzi wa vyuo vikuu wengi kuliko wa awamu zote za kabla yake ukichanganya pamoja.
5. Waalimu wengi kuliko wa awamu zote za kabla yake ukichanganya pamoja.
6. Huduma ya afya na vifaa vya afya ni bora kuliko za awamu zote za kabla yake ukichanganya pamoja.
7. Watanzania wengi wana kazi kuliko awamu zote za kabla yake ukichanganya pamoja.
8. Viwanda ni vingi kuliko vya awamu zote za kabla yake ukichanganya pamoja.
9. Watalii ni wengi kipindi chake na kipato cha utalii ni kikubwa kuliko vya awamu zote za kabla yake ukichanganya pamoja.
10. Demokrasia ni bora na watu wana uwezo wa kusema wakipendacho kuliko awamu zote za kabla yake ukichanganya pamoja.
Sina uhakika na Elimu yako, lakini ukiwa objective utagundua haya:
1. Maisha magumu kwa mtanzania wa kawaida kuliko awamu zote zilizomtangulia
2. Mfumuko wa bei mkubwa kuliko awamu zote pamoja. Tumia 'SI' unit hii: alichukua nchi sukari kilo ikiwa 550/= sasa 2200/= Bia ilikuwa 650/= sasa 2300/= Huo mfumuko ni karibia asilimia 400!!! upo? Mkapa alichukua nchi sukari ikiwa 350= na daladala 300/=akatoka daladala ikiwa 300/= but hata 100 unapanda!
3. Deni la taifa lililoshuka toka 9.6 Bil. US$ (1995) hadi 6.3 Bil US$ na kuelekea kufutwa (2005) limepanda hadi 27 Bil. US$ hivyo habari ya barabara kujengwa kwa mikopo ya WB na IMF hata wewe na ushungi wako ugeweza tu, yaani kuchukua mikopo kwa masifa bila kujali athari zake kwa nchi!! Tazama sasa debt service inakwenda hadi 50years!!!!!!
4. Shule za kata hizo ni za EL hata yeye anajua, yeye alijaribu zahanati za kata akashindwa! Tusubiri na hizi maabara za Sekondari tuone! Desemba si kesho tu...
5. Waalimu yeboyebo wengi zaidi ya awamu zote. Zamani shule za serikali zilikuwa bora kuliko private, sasa ni kinyume Priate ndiyo bora kisa ....
6. Ufisadi mkubwa kabisa zaidi ya awamu zote ukijumlisha pamoja ukazidisha mara kadhaa, uliona wapi rais anayewaambia wezi wa fedha za umma rudisheni then no action? Awamu ya 4 ni unique bwana!
7. Ujangili na uuzaji madawa ya kulevya mkubwa zaidi ya awamu zote ukijumlisha pamoja, tena familia ya Rais ikituhumiwa kuhusika
8. Kushusha kiwango cha kujitegemea kuliko awamu zote pamoja. Leo safari za rais nje ya nchi haziishi kwnenda kuomba omba. Nchi sasa imerudi kuwa koloni la wafadhili, amesababisha kuendelea kuwa ombaomba
9. Nchi sasa haina maamuzi kabisa kuliko awamu zote, Ulaya ndio wanatuamulia mambo yetu
10. Rais asiyejali kuheshimu matumizi ya fedha za umma kuliko awamu zote. tazama safari zake zinavyofuja hela za walalahoi