Mliokutana mjini nendeni ukweni mkatambulishane

sepema

JF-Expert Member
Jun 13, 2019
591
1,000
Nawasalimu nyote

Rafiki yangu yupo kikazi Dodoma tangu mwaka2013.

Mwaka huo aliripoti kazi na dada mmoja mwenyeji wa Babati.Jamaa kwao ni Tanga. Hapa na pale baada ya miezi kadhaa wawili hawa wakajikuta niwapenzi.

Mapenzi yalivyokolea wakaamua waoane kimjini mjini.Yaani waliishi pamoja bila kwenda kujitambulisha kwa wazazi japo kwa njia ya simu waliwapa taarifa.

Likizo zote walikuwa wanabaki huko Dodoma na pale ilipobidi kwenda nyumbani kila mmoja alienda kwao.
Mwaka2015 wakafanikiwa kupata mtoto wao wakwanza.Hapo Sasa wazazi wa upande wakiume wakalazimisha jamaa ampeleke mtoto nyumban.Kwa kuwa mtoto hawezi kwenda mwenyewe ikawa ndo nafasi Sasa ya jamaa kwenda namkewe.Wazazi wakafurahi kuona mjukuu na mkwe wao.

Miaka mingine ilofuata kila mmoja alikuwa anaenda kwao wakati wa likizo na wasipoenda walikuwa wanabaki wote Dodoma. Mwaka huu jamaa wamebahatika kupata mtoto wao wapili.Upande wa mwanamke nao wakakomaa kuwa wanataka kuona wajukuu pamoja na baba yao.Jamaa akaamua atumie likizo yake hii kwenda ukweni Babati.

Wamefika ukweni wamepokelewa vizuri bila shida yoyote.Baada ya muda anakuja binti wa Kama miaka13 hivi.Amefurahi kweli kuwaona pale lakini zaidi anamchangamkia mke wa jamaa. Baada ya shamrashamra mama mkwe anatoka huko jikoni na kumwambia Yule binti"umefurahi kuwaona wadogo zakoee, nahuyo ndo baba yenu msalimie vizuri".

Nifupishe tu hii stori kwa kusema yule mke wajamaa alikuwa na mtoto aliyemzalia nyumbani kabla hajaenda kikazi Dodoma.Kuzalia nyumbani sio shida,tatizo nikwamba kwa miaka yote aliyokaa na jamaa hakuwahi kumwambia kuhusu yeye kuwa na mtoto nyumbani.Mtoto(binti)yupo darasa la saba mwaka huu.

Usiku badala yakuwa muda wa kubwaga moyo jamaa wakaamua wautumie kwa mazungumzo ya kilichotokea.
Mke wajamaa alikiri kuwa kweli binti ni wakwake Ila alishindwa kumweka wazi jamaa kwa sababu ambazo kimsingi hazikuwa na mashiko.

Jamaa alipanga akae siku mbili tatu ukweni ila amekatisha ziara na karudi Dodoma.Amechanganyikiwa,ameshindwa kukisanua pale ukweni hvyo ametulia akifikiri nini Cha kufanya.

Nimemtuliza jamaa kwani hasira alizokuwanazo siwezi shangaa nikiambiwa kaua na kujiua.Ubaya tu nikwamba pamoja na mkasa huo mzito akifanya mauji polisi watasema chanzo Cha mauaji ni WIVU WA MAPENZI.
Mke bado yupo Babati kwani walikubaliana tangu mwanzo kuwa jamaa angewaacha huko walau wiki mbili.

Wakuu,hili nalo linapitaje kwa huyu rafiki yangu

Ushauri wangu; Kama umekutana naye mjini mkapendana,fanya hima uende kwao...Kuna mengine yamuhimu utayagundua ukifika.

Wasalaam!
 
Nawasalimu nyote

Rafiki yangu yupo kikazi Dodoma tangu mwaka2013.
Mara nyingi sana huwa tunavuna tulichopanda, na huwa tunaona taratibu zilizowekwa ni upuuzi na hazina maana.

Ukweli ni jambo la muhimu kwa wenza ila waoji tunapopita njia za mkato, huwa kuna madhara mengi.
Walivyokutana walipaswa kwenda kwa wazazi, na kufuata taratibu za dini yake, yeye akaona hayo sio muhimu yupo bize.

Kutaka kujiua sio suluhisho, ajue ana makosa na kujiua au kuua ni kosa lingine tena. Amechelewa sana, asemehe na kuendelea na maisha ya ndoa yake. Kumwacha mke wake kwa kigezo cha huyo mtoto aliyemwona bado haitampa nafuu.
 
Asiwe mbinafsi kama anampenda kweli waendelee na maisha
Kosa Lao wote kuishi kisela ndio sababu ya yote hayo
Inauma sana mda wote unajiapiza hutokaa kuoa au kuzaa na single mom

Unakuja Kutana na binti mzuri anakwambia hana mtoto unasema yes hapa nimepata halafu kumbe baadaye unagundua ni single Maza
Kwa sisi wanaume uongo kama huo sidhani kama jamaa atakuja kuwa naye sawa ile 100%
 
Tatizo liko wapi sasa,kwani wamesema amchukue mtoto akamsomeshe au? Si wamwache hapo waendelee na maisha Yao....Yeye kumzalisha Binti was watu bila ndoa Wala kutambulika hakukosea au?
Yeye alikuwambioni kufunga ndoa.Hata hvy anachosikitika nikutoambiwa mapema.Mwenyewe anadai angeambiwa mapema Wala asingekuwa na tatizo
 
Inauma sana mda wote unajiapiza hutokaa kuoa au kuzaa na single mom

Unakuja Kutana na binti mzuri anakwambia hana mtoto unasema yes hapa nimepata halafu kumbe baadaye unagundua ni single Maza
Kwa sisi wanaume uongo kama huo sidhani kama jamaa atakuja kuwa naye sawa ile 100%
Penzi limeingia dosari japo jamaa nahisi hatamuacha huyo dada.Maumivu lazima yawepo
 
Hivi mwanamke wa ukanda huo anawezaje kua na mtoto na usijue..ukizingatia huko Manyara wanawake wao wakishazaaga tu matumbo hua yana kua makubwa na kua na kitambi cha kiaina
Labda hakuwa nahuo utaalam wa kuwachunguza
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom