stella1975
JF-Expert Member
- Nov 25, 2018
- 870
- 1,249
Moja ya mikutano ya mkuu wa nchi huko mbeya alijitokeza mama mmoja akidai kuwa Mtoto wake alilawitiwa na mtu mmoja huko, Halafu mtu huyo hajachukuliwa hatua yoyote, kitu ambacho kimemfanya mama huyo kuomba msaaada kwenye taasisi zinazohusika pasipo kupata msaaada na kuomba mkuu wa nchi kusaidia ili mama apate haki, suala ambalo mkuu wa nchi aliamua kulifuatilia, Lakini baada ya mkuu kufuatilia inasemekana kuwa wamepewa majibu kuwa mtuhumiwa alishafungwa kifungo cha maisha, sasa je hili ni IGIZO au ni suala la kweli? Na Kama ni kweli ilikuwaje huyo mama akashindwa kujua kuwa mtuhumiwa alishafungwa? Na huyo mtuhumiwa ni Nani na anafanya shughuli gani?