Mlioko kwenye ndoa mnashindaje hili jambo?

Mlioko kwenye ndoa mnashindaje hili jambo?

Deva

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
1,238
Reaction score
1,819
Salam wanaJf

Wanandoa mnawezaje kuishi na wenzi wenu kwa muda mrefu, mwenzi ambaye amekuzwa kwao huko, mpo tofauti kitabia na makuzi, mnawezaje kuvumiliana. Nimeuliza hili jambo ili ambao bado hatujaoa tusije wachoka wake zetu tukawafukuza bure.

Ilikuwa ni siku moja nimeweka appointment na mwanadada mmoja kuwa atakuja kushinda weekend nyumbani kwangu (nimepanga), mawasiliano yalikwenda vizuri mpaka alipofika, tulikaa vizuri ila baada ya muda nikaanza kuhisi kero, maana kuna mambo alikuwa anafanya mimi sipendelei kabisa.

Nilipokuwa nakula naye nilihisi siko sawa maana mwenzangu anatafuna bila kufumba mdomo, halafu anatafuna kwa sauti( siipendi hii tabia).

Mpangilio wa vitu ndani utabadilishwa uwe kama anavyotaka yeye, hapa nikachoka kabisa, yaani utaratibu wa maisha unabadilika kabisa.

Asubuhi tumeamka nasikia mtu ana vuta makohozi kwenye koromeo cha ajabu hamalizi, kumbe huwa ni utaratibu wake kila akitaka kuswaki, nikajikaza.

Kwa kuwa alikuwa ni girlfriend nilivumilia muda ulipokwisha aliondoka.

Hivi mnaishije wanandoa bila kuchukizana na keroa kutoka kwa wenzi wenu? na sisi mabachela tujifunze kutoka kwenu?

Mimi ninahisi hii amani na furaha niliyonayo itaisha siku hiyo hiyo nitakapooa maana yataka moyo.
 
Nashukuru umejua kuwa mmelewa tofauti mila, desturi dini ila nakusisitizia
Upendo Devion, Upendo baba, upendo huvumilia, upendo husamehe,upendo hufundisha,huleta heshima,upendo jamani nakazia tena upendo.
OA MWANAMKE UNAYEMPENDA.
 
POVU RUKSA WAKUU
ndio maana wazungu wanaruhuusu watoto wao wakifika miaka 16 kuwa na GF na BF,muanze kuzoeana mapema,lkn Bongo mtu una 35 unapata mwanamke ana 30 yaani lazima kusumbuana .Mwanamke kuna vitu hutakiwi kufanya kujichokonoa puani na vidole, sijui unakula huku unaongea,kutafuna vizuri (table manners ni muhimu sana kwa mtoto wa kike),kuwa mbishi,kutema tema mate njiani nk.Kama huwezi kuvumilia inabidi uwe unamwambia kila mara,yaani ukimwambia kitu mara 10 hasipobadilika huyo kimbia babu.
MTOTO WA KIKE UNATAFUNA KAMA JENERETA?,KWACHA KWACHA KWACHA KWACHA KWACHA KWACHA.
 
Mapenzi ya dhat huficha madhaifu ya mwenzako

Ya kama ww unampenda mtu flan hata kama uyo mtu ni dhaifu kias gan lazma utampenda tuu kwa sabanu hayo ndio mapenz ya dhat

Mambo mengine yanayoteka katika ndoa ni uvumilivu tuuu na uthubutu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkeo atakuwa /atakuja kuwa na Bahati sana
 
POVU RUKSA WAKUU
ndio maana wazungu wanaruhuusu watoto wao wakifika miaka 16 kuwa na GF na BF,muanze kuzoeana mapema,lkn Bongo mtu una 35 unapata mwanamke ana 30 yaani lazima kusumbuana .Mwanamke kuna vitu hutakiwi kufanya kujichokonoa puani na vidole, sijui unakula huku unaongea,kutafuna vizuri (table manners ni muhimu sana kwa mtoto wa kike),kuwa mbishi,kutema tema mate njiani nk.Kama huwezi kuvumilia inabidi uwe unamwambia kila mara,yaani ukimwambia kitu mara 10 hasipobadilika huyo kimbia babu.
MTOTO WA KIKE UNATAFUNA KAMA JENERETA?,KWACHA KWACHA KWACHA KWACHA KWACHA KWACHA.
Nimeandika nikafuta nikaandika nikafuta...
Umenena vyema kabisa.
 
Back
Top Bottom