Sunbae
JF-Expert Member
- Sep 14, 2015
- 254
- 176
Anaandika Dotto Burendu
1.Kiwanda cha nyama Shinyanga na Dsm
2.Kiwanda cha Maziwa Utegi
3.Kiwanda cha nyuzi Tabora
4.Kiwanda cha matairi Arusha
5.Kiwanda cha viberiti Moshi
6.Kiwanda cha dhana za kilimo Mbeya
7.Kiwanda cha Magunia Iringa
8.Kiwanda cha nguo Musoma na Mwanza
9.Kiwanda cha viatu cha bora
10.Kiwanda cha kuunganisha magari cha Dsm
11.Kiwanda cha Sigara cha Morogoro.
12. Kiwanda cha Ngozi cha Ilemela Mwanza.
13.Kiwanda cha Redio Arusha n.k.
Tuambueni mliweza vipi kuwasomesha bure vijana kama akina Joseph Warioba,Issa Shivji,Marehemu Samwel Sitta,Jakaya Kikwete,Edward Lowasa na wengine wengi pale chuo kikuu Dsm tangia kikiwa Lumumba mpaka mkakipeleka Mlimani?.
Leo uwezo wetu kuwasomesha vijana ni mdogo,mliwezaje kugharamia elimu ya vijana wetu bure kuanzia Elimu ya msingi mpaka chuo kikuu?mkawapa kalamu,madaftari,na uji,Sekondari mkawalipia mpaka nauli,chuo kikuu mkawapa na nauli!
Huwa naambiwa eti watu walikuwa wachache,lakini mbona GDP,GNP na National Income ilikuwa kiduchu,haikufika hata Trilioni moja,leo watu wanaongezeka na mapato yamepaa kweli,kwa sasa tunatarajia kukusanya Trilioni 29,tumekwama wapi?
Nakumbuka usafiri wa Treni ulikuwa wa uhakika,mkafungua mpaka vyuo vya TRC pale Tabora na Morogoro,nakumbuka watu walisoma bureeee,leo tuna wasomi wengi kweli kweli usafiri ni shida!.
Nakumbuka Marehemu baba yangu aliniambia kuwa nchi ilikuwa na ndege kubwa kweli kweli tena Boeng 737,ndege zilifika 14,leo zipo sijui nne tu,namshukuru Rais Magufuli kwa kutuondolea aibu hii,sasa tuna Bombadier,ninyi mliwezaje kufikisha ndege 14 miaka ya sabini wakati huko tukiwa na vyuo vikuu viwili tu,cha Dsm na SUA,leo tunavyuo vikuu zaidi ya 50,haya mambo yameshindikana!.
Natamani kuisikia sauti ya Julius Nyerere atupe siri ya kukifanya chuo kikuu cha Dsm kuwa sehemu ya mijadala,kila kiongozi mkuu wa nchi yeyote alipokuja nchini,alipangiwa ratiba ya kwenda kutoa mhadhara pale Nkrumah hall,sababu hasa ilikuwa ni nini?leo haya mambo huwezi yaona vyuo vikuu,wanaambiwa waache siasa,vyuoni si sehemu ya siasa,hata vyuo vinavyofundisha sayansi ya siasa hakuna mihadhara ya wanasiasa,wewe Julius kwa nini ulipenda kuona mihadhara ya kutosha chuo kikuu?
Watoto walikuwa wanahisi ufahari kusoma shule za serikali,leo hawataki kwenda huko,ninyi mlifanyaje sababu leo shuke za serikali zipo pabaya,mwaka huu katika shule 100 zilizofanya vizuri kwenye matokeo ya kidato cha nne,serikali zipo saba tu,93 ni binafsi!.
Viwanja vya mpira wa miguu mlijenga ninyi,mlijenga CCM Kirumba Mwanza,Al Hassan Mwinyi Tabora,Kambarage Shinyanga,Gombani Pemba,Jamhuri Morogoro na Dodoma,n.k sasa hivi hatuna uwezo hata wa kuweka nyasi bandia,tunasubiri huruma za FIFA.
Mlijenga leaders club kila mkoa,leo viongozi wetu hawana pa kupumzikia,wanakwenda Pub,tunakumbana nao huko huko!.
Ninatamanani kuona mijadala mikali na huru kuanzia kwenye mitandao ya kijamii,vyombo vya habari,bungeni,vyuo vikuu,mikutano ya vyama vya siasa,Kwenye debate huko mashuleni,ndani ya baraza la mawaziri,kwenye vyama vya siasa,mikutano na vyombo vya habari,tukijadilianankwa hoja,ipi njia sahihi ya kutuvusha hapa?
Wapo wazee wetu walioshiriki kuijenga nchi hii na walishuhudia ikiyumba ,naamini wanachakutuambia,wapo Akina Ibrahim Kaduma,Joseph Warioba,Salim Ahmed Salim,John Malecela,Edwin Mtei,Kingunge Ngombale,Hassan Moyo,Issa Shivji,Damian Lubuva,Ally Hassan Mwinyi,Fortunatus Masha,Maalim Seif,Hamad Rashid,n.k
Semen wazee wangu,tuambueni pale tulipoangukia ili tusije tudia tena,vijana huku leo hawataki kupishana kwa hoja,nikutuhukiana wao kwa wao,huku ajira zikiwa hakuna,mashamba makubwa yote yamekufa,kuanzia Karatu mpaka Morogoro na Tanga.
Wazee semeni tu kwa unyenyekevu,vijana watawasikia,sisi kwa sisi hatusikilizani,tumebaki kutishana ,kutunishiana misuli na maneno ya kudhalilishana kwa sababu tu tunapishana misimamo na mitazamo ya namna ya kutoka hapa!.
Wazee zungumzeni,muwaweke vijana na hata viongozi wetu kwenye njia sahihi,msikae kimya,lisaidieni taifa hil.
Nikifurahi kuwasikia kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Azimio la Arusha,nilifurahi sana,hebu semeni sana,wapi kama taifa tuliteleza na katu tusije fanya kosa,wapi tupaenzi?
Tukumbuke ajenda yetu ni Tanzania ya viwanda,haya mengine yanatokea tu.
Wasalaam.