Mlio Nyakijoga- Mugana, Bwanjai wilaya ya Misenyi kuhiji tunaomba kinachojiri

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
40,402
74,004
Leo kuna HIJA sehemu inaitwa NYAKIJOGA-MUGANA PARISH iliyopo kata ya Bwanjai, tarafa ya Kiziba wilaya ya Nkenge.

Ilianza jana kwa mkesha wa Hija. Papa aliibariki na kuwa Lurdi ya Tanzania na hivyo kuwa na hadhi ya watu kwenda kuabudu kwa Hija.

Mliopo hapo tunaomba kinachojiri tafadhali!
 
Kutoka mugana misenyi kagera
FB_IMG_16036335205049888.jpg
FB_IMG_16036335241207907.jpg
FB_IMG_16036334996061922.jpg
FB_IMG_16036334757653489.jpg
FB_IMG_16036335277710208.jpg
FB_IMG_16036335313116884.jpg
FB_IMG_16036334797562192.jpg
 
Halafu mkitoka hapo mnaenda kunywa pombe hadi mjikojolee. RC bhana eti kunywa kidogo sasa kreti zima ndio kidogo?

Eti kunywa ila usitende dhambi sasa hao mabaamedi mnaowashikashika baada ya kulewa sio dhambi?
 
Kwa kauli yako Akishakunywa akalewa anajikojolea yeye au anakukojolea wewe.? Na akimshika baamedi wewe ni sehem gan ya mwili wako inayoumia??
Anakuwa ametenda dhambi gani akinywa mpaka akajikojolea???
Je Wewe ambaye hunywi u mtakatifu??
Na pia unawaongeleaje wale wanaokunywa mbili tatu then wanaenda makwao..wanakua wametenda dhambi gani??
 
Halafu mkitoka hapo mnaenda kunywa pombe hadi mjikojolee. RC bhana eti kunywa kidogo sasa kreti zima ndio kidogo?

Eti kunywa ila usitende dhambi sasa hao mabaamedi mnaowashikashika baada ya kulewa sio dhambi?
nani alikwambia kunywa pombe ni dhambi??
 
Sa
Leo kuna HIJA sehemu inaitwa NYAKIJOGA-MUGANA PARISH iliyopo kata ya Bwanjai, tarafa ya Kiziba wilaya ya Nkenge.

Ilianza jana kwa mkesha wa Hija. Papa aliibariki na kuwa Lurdi ya Tanzania na hivyo kuwa na hadhi ya watu kwenda kuabudu kwa Hija.

Mliopo hapo tunaomba kinachojiri tafadha
Leo kuna HIJA sehemu inaitwa NYAKIJOGA-MUGANA PARISH iliyopo kata ya Bwanjai, tarafa ya Kiziba wilaya ya Nkenge.

Ilianza jana kwa mkesha wa Hija. Papa aliibariki na kuwa Lurdi ya Tanzania na hivyo kuwa na hadhi ya watu kwenda kuabudu kwa Hija.

Mliopo hapo tunaomba kinachojiri tafadhali!
Hiyo sehemu ilibarikiwa na papa huyu huyu aliyebariki ndoa jinsia moja au kuna mwingine?
 
Kuna tukio gani lilitokea hapa mpaka kupelekea kupata baraka za Papa kuwa sehemu ya hija?

Utanisamehe nimekuwa mvivu kufanya concise summary, nimetape maandiko ya watu , lkn ni ya kweli

Pata kuijua historia ya Nyakijoga​

30 October 2011

HISTORIA FUPI YA NYAKIJOGA KWA UTAFITI a kituo cha Hija cha Parokia ya Mugana.
Wakati huo Parokia ya Mugana ilikuwa ikijiandaa kuadhimisha Jubilei ya Miaka 50 tangu ilipoanzishwa. Jubilei ilikuwa iadhimishwe mwaka 1955. Kituo hiki cha Hija kilianzishwa kwa madhumuni ya kushiriki kiroho katika maadhimisho ya Jubilei ya miaka 100 tangu tamko rasmi la Kanisa la mwaka 1854, kuwa ni nguzo ya imani kwamba Bikira Maria aliumbwa bila dhambi ya asili. Vilevile, mwaka 1958 kuliadhimishwa Jubilei ya miaka 100 tangu Bikira Maria mwenyewe alipomtokea msichana Bernadeta Subiru huko Lurdi Ufaransa mwaka 1858 na kujitambulisha kuwa yeye ndiye “aliyeumbwa bila dhambi ya asili”
Kwa kujitambulisha hivyo Bikira Maria athibitisha ukweli ambao ulikuwa unakubaliwa na Kanisa katika mapokeo yake ya kawaida (Tradition), ambao ulitamkwa rasmi na Kanisa mwaka 1854.
Ili kuwawezesha waumini wote wa Jimbo la Rutabo la nyakati zile kushiriki kikamilifu, Mwashamu Laureani Rugambwa, alimwomba Baba Mtakatifu Pio XII awaruhusu wote watakao Hiji hapa wapate rehema za Jubileo hiyo kuu ya Lurdi. Baba Mtakatifu aliruhusu.

.......................................................

Ijue Nyakijoga, Mugana, Kiziba, Bukoba, sehemu ya kuhiji ibada za Bikira Maria. Mwanzilishi ni Kardinali Rugambwa. Alipendelea kuhiji kwa Bikira Maria kule Leuge Ulaya. Lakini baadae alimwomba Pope John kupata sehemu ya kuhiji Afrika. Pope alikubali na safari ya kutafuta ikaanza. Kardinali alibaini sehemu ya Mugana iliyokuwa inatiisha kwa miamba yake kama mizizi na maji kuchipukia humo pangoni. Palitengenezewa sanamu ya Bikira Maria na Kanisa. Watu walianza kuhiji toka pande za dunia hadi leo hii. Hudaiwa hata maji toka pale yana miujiza ya mama Maria. Kwenye miaka ya sitini nilihiji nikiwa mkatoriki, lakini kwa sasa mimi Mpentekoste, siwezi kwenda tena eg Zaburi 115, 146 na Kutoka 20 nk . Soma kitabu cha maisha ya Mhadhama Kardinali Rugambwa toka Bukoba
 
Asante sana sikufahamu hii historia hii. Ninakwenda Lourdes Na Fatima pia.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom