Mlango wa Kutokea

happiness win

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
2,461
1,384
Nimewasikia Akinamama waliokuja kumfariji shangazi yangu baada ya mume wake kutafuta nyumba ndogo na kuelekeza nguvu zote huko wakimfariji na kumwambia “kila jaribu lina mlango wake wa kutokea, jipe moyo Mungu atakusaidia” Sasa najiuliza, vipi kuhusu mlango wa kuingilia? Wamama hawa wanazijua fika tabia za ugonvi, uvivu, umbeya na nyingine nyingi alizonazo Shangazi yangu. Sasa iweje leo wanapoteza nguvu kwa kukesha, kulia na kuomba kutafuta mlango wa kumtoa Shangazi kwenye majaribu! Kwa nini hawakumtahadharisha Shangazi kufunga mlango wa kuingilia kwenye hayo majaribu?
Wewe unaonaje kuhusu hili?
 
Wewe pia unalazimika kumjuza huyo mama mabaya kama unazijua tabia zake kwanini hukuchukua hatua ya kumtahadharisha.
 
Imekuwa vigumu kwangu kumkalisha shangazi yangu mtu mzima na kumuonya kwa tabia zake kwa kulinda ndoa yake. Hao wamama anao siku zote kwenye vikundi vyao, nadhani ni rahisi kwao kama wangeamua kumuonya siku nyingi.
 
Hapa dada mlango wa kutokea shangazi yako ni huohuo alioingilia...Huwezi kumwambia(siyo heshima) mtafute mmojawapo wa hao kina mama umweleze umegundua mlango then umpasulie mwanzo mwisho tabia za shangazio-kisha umwambie na solution plan ambayo ndo maujanja ya kumkeep husband wake @home...hapo uconclude kwa kumwambia aichunguze nyumba ndogo vizuri bila kinyongo(hapa atumie mbinu iitwayo...Keep you friends close but keep your enemies closer so that when you stab it goes deeper), agundue maujanja yaliyotumika then aongezee maujanja uliyomfundisha ww...@last shes on top of the world-problem solved!
 
Asante Edcv.

Kwa wakati huu huyo shangazi na wamama wengine wamejichimbia hawali, hawanywi wanakesha kwa maombi. Ninaamini maombi yanafanya kazi lakini naona kama wanapoteza muda.
 
Asante Edcv.

Kwa wakati huu huyo shangazi na wamama wengine wamejichimbia hawali, hawanywi wanakesha kwa maombi. Ninaamini maombi yanafanya kazi lakini naona kama wanapoteza muda.
Hapana sasa ndo maombi yanafanya kazi hivyo na wewe ndiye mtumishi aliyeshushiwa solution(hongera!) go for it!
 
Pamoja na kujua maombi yanafanya kazi, ni vema tukawa wajanja wa kutojiingiza kwenye majaribu. Ukiachia mwanya mambo yakatokea inaleta shida. Sasa nyumba ndogo inapeta, shangazi yangu anashinda njaa akilia na kuomba, mweeee!
 
Back
Top Bottom